Vodacom mdhamini mkuu Mashindano ya Gofu
Vodacom mdhamini mkuu mashindano ya Gofu

Dar es Salaam: Vodacom Tanzania Plc imesaini mkataba na Chama cha Gofu Tanzania, huku kampuni hiyo ya mawasiliano ikijitokeza kuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open, yanayotarajiwa kushirikisha wachezaji zaidi ya 150 kutoka ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Ushirikiano huu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuendeleza michezo ya gofu katika msimu wa tatu hapa jijini Dar es Salaam na visiwani Zanzibar.
Vodacom ikiwa inaadhimisha miaka 25 inalenga kujikita kama mtandao namba moja unaounga mkono mchezo wa gofu nchini Tanzania.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuwa jukwaa la kuibua vipaji, kuendeleza mshikamano katika michezo na ubunifu wa kidijitali.
Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano haya, mkuu wa idara ya masoko na uwezeshaji Vodacom Business, Joseph Sayi, alisema:
“Ushirikiano wetu na Tanzania Open unaonyesha dhamira ya Vodacom katika kukuza michezo nchini Tanzania huku tukionesha namna teknolojia inavyoweza kuboresha maisha ya wananchi hata kupitia michezo. Kuanzia huduma za mtandao hadi huduma za malipo kwa kutumia M-Pesa, tunahakikisha kila mmoja anapata uzoefu wa kipekee ndani na nje ya uwanja.”
Naye mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania, Gilman Kasiga, alisema kuwa
Mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2025 ni tukio la kihistoria kwa mchezo wa gofu na kwa taifa.
“Vodacom Tanzania Open siyo tu jukwaa la kuonesha umahiri wa wachezaji wetu wa kulipwa na wale wa kiwango cha juu, bali pia ni chanzo cha hamasa na matumaini kwa kizazi kipya cha wachezaji,” alisema.
“Mashindano haya ni ya ubora wa kimataifa, na tunawaalika wadau wote wa gofu pamoja na umma kushiriki nasi katika kusherehekea mchezo huu wa heshima na hadhi ya kipekee
Kwa kuhitimisha, Mkuu wa idara ya masoko na uwezeshajiVodacom Business, Joseph Sayi alieleza.
Alieleza kuwa Vodacom Tanzania Open ni mfano halisi wa kuunganisha urithi wa michezo na ubunifu wa teknolojia ya kisasa. Sisi Vodacom tunajivunia kuwa sehemu ya mashindano hayo.
Soma: Washindi wa gofu wapewa tuzo Dar
”Ushirikiano kati ya Vodacom Tanzania na Chama cha Gofu Tanzania ni hatua kubwa katika kuimarisha nafasi ya Tanzania kwenye ramani ya gofu ya kikanda, huku ikisukuma mbele dhamira ya Vodacom ya jamii iliyounganishwa kidijitali,” meneja huyo alisema.