Vyama viwili vyajitangazia ushindi urais

MALAWI : VYAMA vya siasa vinavyowaunga mkono wagombea wakuu wa urais nchini Malawi vimejitangazia ushindi kabla ya Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo rasmi.
Vyama hivyo ni Malawi Congress Party (MCP) kinachoongozwa na Rais wa sasa, Lazarus Chakwera, na Democratic Progressive Party (DPP) kinachoongozwa na rais wa zamani, Peter Mutharika, ambavyo vyote vilitoa taarifa kuwa wagombea wao wameshinda.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Annabel Mtalimanja, amesema tayari kura zimehesabiwa kwa zaidi ya asilimia 99, lakini akasisitiza kuwa matokeo rasmi bado hayajatangazwa. Amesema tume haitahairisha mchakato huo na kuvitaka vyama na wagombea kuheshimu taratibu zilizowekwa za kutangaza matokeo.
Uchaguzi huo wa Jumanne ulitajwa kuwa na ushindani mkali kati ya Rais Chakwera na Mutharika, ambaye aliondolewa madarakani katika uchaguzi uliopita. SOMA:Uchaguzi Mkuu Malawi kufanyika leo