DAR ES SALAAM :OFISI ya Rais Mipango na Uwekezaji imeshauri vyama vya siasa kuweka Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 kuwa sehemu ya ilani za vyama ili kuwa na muelekeo mmoja na kufanikisha malengo ya dira hiyo.
Pia viongozi wa vyama vya siasa nchini vimeshaurikuwe na elimu ya kodi ili kuondoa sintofahamu kati ya walipokodi na serikali na kueleza kuitaka dira hiyo kuainisha sheria kali juu ya masuala ya rushwa kwani yanarudisha nyuma taifa na ukosefu wa haki.
Hayo ameyasema leo katika Mkutano wa Vyama vya Siasa kuhakiki Rasimu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 Dar es salaam kujadili juu ya mambo ya kuongezwa na kutiliwa mkazo katika dira ili kuwa na mlengo unaofanana kwa vyama vyote.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof Kitila Mkumbo alisema dira ya Maendeleo ni ya Taifa na sio ya serikali na ndo sababu kubwa ya wameanza na viongozi wa vyama vya siasa katika uhakiki wa dira hiyo.
Prof Kitila amesema wanasiasa hawatakiwi kutofautiana wala kupishana katika mikakati ya maendeleo ya taifa kwa sababu chama chochote kinaweza kupata nafasi katika utekelezaji wa maendeleo na asilimia kubwa ya mambo yaliyowekwa katika dira ni mawazo na maoni waliyoyatoa kwenye kikao walichokifanya Agosti 21,mwaka huu.
“Sisi wanasiasa tusipishane kwenye safari ya maendeleo, hata nchi za wenzetu hawapishani mahali wanapokwenda lakini wanapishana katika mikakati ya kuwafikisha wanapokwenda sisi katika mfumo wa vyama vingi unakuta bado tunapishana nashukuru kwamba hilo tunauwezakano tukafika,” amesema Prof Kitila.
Aliongeza dira hiyo imeundwa kwa miundo minne na msingi mkuu wa dira ni amani, usalama na utulivu na mkondo huo upo mikononi mwa wanasiasa kwa sabbau wananguvu kubwa katika kuleta amani au kuivunja.
Aidha, aliahidi kufanyia kazi maoni ya wanasiasa hao katika rasimu ya pili itakayotolewa mwakani kabla ya kukabidhiwa kwa serikali ili kupitishwa katika bunge, aliongeza kuwa Desemba 18, mwaka huu atakuaa na mkutano na vijana ili kujadili dira hiyo kwa upande wao.
Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof Ibrahim Lipumba aliunga mkono hoja hiyo na kusema kuwa ni jambo la msingi na kuahidi kulituma kwa waandaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2025 kuzingatia mambo yaliyopo katika dira kwa sababu dira imezungumzia demokrasia na katiba liwekwe katika utekelezaji wa haraka
“Nimelituma kwa aatu ambao wanaandaa ilani yetu ya uchaguzi ya mwaka 2025 kwamba kuna mambo ya msingi ya kuweza kuzingatia kuweza kuonesha kwamba chama kinachosimamia haki sawa kwa wote kitatekelezaji mambo muhimu, kwajiyo agizo lako kwamba sisi kama vyama tunatakiwa kushiriki katika kutoa michango katika dira hii basi tuweze kuitumia katika kutumia ilani zetu,” alisema Prof Lipumba.
Pia alisema kuwepo na mkakati wa kuweza kupambana na jambo la elimu kwenye uchangiaji wa kodi, kwani kunaonekana kuwa na sintofahamu japokuwa kuna mikakati inawekwa lakini pesa zinaonekani hazitoshi japokuwa kodi zinakusanywa na kwa walipa kodi nao wanalalamika kuwa kodi ni kubwa hivyo kuwa hivyo kukiwa na elimu juu ya suala hilo itasaidia kuondoa hiyo mkanganyiko huo.
Kwa upande wake Isihaka Mchinjita Makamu Mwenyekiti ACT Wazalendo Bara ametoa maoni yake kwa kusema dira 2050 iwe na mapinduzi ya viwanda kwa sasa.