Waandishi wanolewa matumizi ya takwimu

DAR ES SALAAM; CHUO cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kimewataka waandishi wa habari kutumia takwimu sahihi katika kazi zao, ili kuboresha utoaji wa taarifa na kuondoa upotoshaji unaojitokeza mara kwa mara katika jamii.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri wa Chuo hicho, Prof. Ahmed Mohammed Ame, alitoa rai hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa chuo hicho.

“Waandishi wa habari mkiziandika taarifa zenu kwa kutumia takwimu sahihi, habari zenu zitakuwa nzuri na zenye kuvutia zaidi. Lakini waandishi wasio na elimu ya takwimu mara nyingi taarifa zao hazijakaa vizuri,” alisema Prof. Ame.

Amesema kwa sasa matumizi ya takwimu ni makubwa huku akitolea mfano mkutano wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walivyotumia takwimu wakati wakielezea maendeleo ya miaka mitano kwa lugha rahisi kwa kutumia picha na graph

Aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kusimamia chuo hicho na kukitumia katika masuala mbalimbali ya kitaaluma, akibainisha kuwa nchi jirani ikiwemo Somalia pia zimekuwa zikikitegemea kwa kuwajengea wananchi wao uwezo kupitia mafunzo ya kitaalamu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Tumaini Katunzi, alisema kesho chuo hicho kitasherehekea miaka 60 tangu kuanzishwa kwake, hivyo waliamua kutumia maadhimisho hayo kuwaelimisha waandishi wa habari kuhusu matumizi ya takwimu katika uandishi wa habari.

“Kumekuwa na upotoshaji mkubwa katika jamii kwa sababu kila mtu anajihisi ni mtakwimu ilhali hana uelewa sahihi. Hivyo elimu hii itasaidia waandishi kuongeza ujuzi na kuleta mabadiliko chanya,” alisema Dk. Katunzi.

Alisisitiza umuhimu wa kuendeleza elimu katika taaluma ya uandishi, akibainisha kuwa tasnia hiyo imevamiwa na watu wasio na sifa, jambo linalohitaji kupatiwa ufumbuzi kwa kuongeza ujuzi kupitia mafunzo endelevu.

Habari Zifananazo

2 Comments

    1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

      HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button