Wadau wa kilimo Afrika kukutana Tanzania

TANZANIA imetajwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Zana Endelevu za Kilimo Afrika (Africa Sustainable Agricultural Mechanization), utakaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Februari 3 hadi 6, 2026, sambamba na uzinduzi wa Mkakati wa Taifa wa Zana za Kilimo Awamu ya Pili.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema mkutano huo unafanyika kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Kilimo ya Tanzania na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO).

Katika mkutano huo utaweza kuonyesha  fursa zilizopo kwa nchi za Afrika, kubadilishana uzoefu, kuimarisha ushirikiano na kuharakisha matumizi ya zana za kisasa za kilimo kwa lengo la kufanya mageuzi endelevu ya sekta ya kilimo Barani Afrika.

Aidha, Chalamila amesema kupitia mkutano huo, Waziri Mkuu atazindua Mkakati wa Taifa wa Zana za Kilimo Awamu ya Pili, ambao utakuwa mwongozo mkuu wa kuongeza tija ya kilimo kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa. SOMA: Bunifu za kilimo zapewa kipaumbele bajeti 2026/27

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Charles Tulai, amesema  mkutano huo ni muhimu katika kusaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabianchi na ongezeko la watu.

Amesema Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na mazingira yake mazuri na jitihada zake katika kuendeleza sekta ya kilimo, huku vijana wakitajwa kuwa nguvu kazi muhimu katika kufanikisha maendeleo ya kilimo Barani Afrika.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button