Wadau wakutana Nairobi kujadili changamoto za wakimbizi Afrika

NAIROBI, KENYA: Mkutano wa siku mbili unaowaleta kwa pamoja muungano wa Amahoro, Inkomoko na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) umeanza leo (April 28, 2025) jijini Nairobi, Kenya, ukiangazia changamoto zinazowakabili wakimbizi barani Afrika (AFD2025).

Ukiongozwa na kaulimbiu ‘wote ndani’ (siyo rasmi), mkutano huo unawakutanisha viongozi kutoka sekta binafsi, serikali, mashirika ya hisani, na jamii za wakimbizi ili kuharakisha suluhisho za ujumuishaji wa kiuchumi na mshikamano wa kijamii barani Afrika.

Inaelezwa kuwa takribani watu milioni 45 waliolazimika kuhama makazi yao barani Afrika, hivyo AFD2025 inangazia umuhimu wa ujumuishaji, uwekezaji, na ubunifu katika kufungua fursa kwa watu waliopoteza makazi na jamii zinazowahifadhi.

“Jamii za wakimbizi zina ujuzi, vipaji, na ari ya kuchochea ukuaji wa uchumi na uvumbuzi,” alisema Nancy Aburi, Mkuu wa Ushirikiano na Sekta Binafsi Afrika katika UNHCR. “Kupitia AFD2025, tunadumisha ushirikiano unaowekeza katika uwezo wao na kutoa suluhisho za kudumu zinazoongozwa na soko.”

Mkutano huo unajumuisha soko maalum litakalowezesha wajasiriamali kutoka kwa jamii za wakimbizi na wenyeji kuonyesha bidhaa zao, vipindi vya majadiliano ya ngazi ya juu pamoja na viongozi kama James Mwangi (Equity Group Holdings), Reeta Roy (Mastercard Foundation), na Kelly Clements (Naibu Kamishna Mkuu wa UNHCR), pamoja na wajasiriamali wakimbizi wakiwemo Bereket Goitom (Canaan Group).

“Wajasiriamali na jamii za wakimbizi tayari wana vipaji na ustahimilivu. Wanahitaji tu upatikanaji wa haki wa masoko na mitaji,” alisema Julienne Oyler, Mwanzilishi Mwenza na Mkurugenzi Mtendaji wa Inkomoko. “Katika AFD2025, tunatoa wito kwa sekta binafsi kuchukua hatua kwa suluhisho na uwekezaji wa kweli ambao utaleta athari ya kudumu.”

Mkutano huo utahitimishwa kwa hafla maalum ya Mahafali ya Amahoro Fellowship, ikiadhimisha kundi la kwanza barani Afrika la viongozi waliopitia uzoefu wa kuhamishwa kwa lazima.

“AFD2025 ni wito wa kuchukua hatua,” alisema Isaac Kwaku Fokuo, Mratibu wa Muungano wa Amahoro. “Unatuhamasisha sote: wafanyabiashara, serikali na jamii kuwa ‘All IN’ kwa wakimbizi, si kwa hisani, bali kwa kuwapatia fursa.”

Muungano wa Amahoro ni jukwaa linalowaunganisha viongozi wa sekta binafsi barani Afrika kwa ajili ya athari chanya za kijamii. Tunatoa suluhisho maalum kwa sekta binafsi, kuwawezesha kunufaika na rasilimali watu barani Afrika, ikiwemo katika mazingira hatarishi kama jamii za wakimbizi. Pia tunawawezesha vijana wa Afrika, wakiwemo wale kutoka jamii zilizohamishwa kwa lazima, kupitia uhusiano wa kimkakati na sekta binafsi ili kuunda fursa za pamoja kwa wote.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button