Wafanyabiashara tumieni fursa za uchaguzi

DODOMA : WAJASIRIAMALI wametakiwa kujipanga kufanya biashara wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu kwenye maeneo yao ili wajiinue kiuchumi.

Ofisa Uendelezaji Biashara Mwandamizi kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) Mkoa wa Dodoma, Crispin Kapinga aliwataka wajasiriamali kutumia mikutano ya kampeni itakayofanyika kwenye maeneo yao kufanya biashara. “Siasa na uchumi vinakwenda pamoja, ni vyema wakatumia fursa hiyo kufanya biashara,” alisema Kapinga.

Kapinga alisema fursa nyingi zitatokea hivyo si vyema wajipange kufanya biashara sambamba na kuhakikisha bidhaa wanazozalisha zinakuwa na ubora. “Dunia inabadilika, elimu imetolewa sasa kazi yao ni kuboresha bidhaa, kufuata misingi ya afya na usafi katika utengenezaji bidhaa na kila mmoja kutambua ana jukumu la kulinda afya za walaji,” alisema.

Akizungumzia maonesho ya kilimo, mifugo na uvuvi maarufu Nanenane 2025 yaliyomalizika hivi karibuni Kapinga alisema ya mwaka huu yameboreshwa kwa kiwango kikubwa. “Mwaka huu maonesho yalikuwa na maboresho makubwa yaliyovutia waoneshaji na hata waliotembelea kujifunza na kupata elimu mbalimbali, miundombinu mingi ya ndani hasa barabara zilifanyiwa maboresho makubwa,” alisema.

SOMA: INEC yawataka wasimamizi kufuata sheria.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button