Wafugaji Kaskazini Wahimizwa Kuchanja Mifugo

WAKALA ya Maabara ya Vetenari Tanzania (TVLA) Kanda ya Kaskazini wamewashauri wafugaji kanda hiyo kuhakikisha wanaipa chanjo mifugo yao ili kuikinga na magonjwa.

Rai hiyo imetolewa na Meneja wa TVLA Kanda ya Kaskazini, Dk Rowenya Mushi wakati akisisitiza umuhimu wa chanjo kwa mifugo pamoja na matumizi ya maabara hiyo katika mahojiano na mwandishi wa habari hii.

Dk Mushi amesema endapo wafugaji watachanja mifugo yao wataepuka kutumia gharama kubwa kuitibu au kupata hasara pindi wanapokufa kutokana na magonjwa ya mifugo pamoja na kukosa chanjo sahihi.

Amesema serikali imeweka maabara hiyo ili kuwasaidia wafugaji kuondokana na mikwamo ya magonjwa ya mifugo na uhakiki wa vyakula wanavyokula mifugo huku akitoa rai kwa wazalishaji na wasambazaji wa vyakula vya mifugo kutumia maabara hiyo kupima vyakula hivyo ili kuwa na ubora.

“Mfugaji anaingia gharama kubwa ya chakula lakini chakula kikiwa katika hali duni mifugo haitaleta tija hivyo tunashauri wafugaji watumie chanjo mbalimbali za mifugo zinazozalishwa nchini ili kulinda mifugo kwani sasa hivi chanjo aina saba zinazalishwa nchini ikiwemo mapafu ya ng’ombe, kimeta unaoshambulia mifugo na binadamu, mdondo/kideri na kinga dhidi ya ugonjwa wa kutupa mimba kwa ng’ombe.

Amesisitiza wafugaji kutumia chanjo hizo ikiwemo kuchanja zaidi mifugo yao kwani lengo la kuhakikisha mifugo inakuwa mtaji kwa kuwanufaisha wafugaji na kuwakwamua kiuchumi. SOMA: Serikali bega kwa bega na wafugaji Ngorongoro

Sikujua Magobo ambaye fundi sanifu maabara alisisitiza wafugaji kutumia maabara hiyo kutafiti magonjwa yanayoshambulia mifugo ikiwemo kubaini changamoto za magonjwa yao kwa kupeleka sampuli za mifugo ili kupata dawa sahihi ya kuponya mfugo. “Ukibaini ugonjwa wa wanyama utaokoa gharama kubwa za kuwatibu hivyo wafugaji tumieni maabara hii ili mpate chanjo sahihi za kutibu mifugo yenu na dawa za uhakika,” alisema.

Wakati huohuo, wafugaji akiwemo Juliana John na Samweli Akonai waliwasihi wenzao kuendelea kuchanja mifugo yao na kuwapa malisho/vyakula bora ili waweze kuona tija za ufugaji ikiwemo kupata fursa za ufugaji katika kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi.

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us →→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

  3. Nowadays earning money online is very easy . Eanrs every month online more than $17k by doing very easy home based job in part time u can also do this simple online Job by visiting website

    More Details For Us→→  http://www.job40.media

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button