Wafugaji sasa kufuga kisasa

ARUSHA: TAASISI ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela imekuja na teknolojia ya “Bolus “inayomwezesha mfugaji kufuga kisasa ili kuondoa changamoto wanazokumbana nazo
Kwa mujibu wa mtafiti kutoka chuo hicho Dk, Gladness Mwanga amesema teknolojia hiyo inayojulikana kwa jina la “bolus” inayomsaidia mfugaji kubaini changamoto ya mfugo wake
Amesema teknolojia hiyo inayojulikana kwa jina la tonge au kwa jina la kitaalam kama “Bolus” kwa ng’ombe wa kisasa inamwezesha mfugaji kupata ndama na kujua changamoto za mifugo yake ikiwemo ng’ombe kuwa na joto na kuweza kubeba mimba
Amesema teknolojia hiyo itawasaidia wafugaji kujua changamoto ya mfugo wake ikiwemo ulaji na unywaji wa maji ili kumwezesha mfugaji kupata taarifa sahihi za mifugo yake.
“Kifaa hiki kinamsaidia mfugo wake kupata taarifa kamili anaendeleaje amekula chakula cha kutosha au la,”
“Pia wafugaji wa ng’ombe wa nyama nao wanavalishwa hereni maalum ili kubaini ulaji wa chakula, yupo wapi na pia ametumia muda gani kutembea au kubaini changamoto nyinginezo.



