Wagombea CCM watakiwa wasivimbe vichwa

TANGA; Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahaman amewaasa wagombea nafasi za ubunge na udiwani mkoani humo kuacha majivuno badala yake wajikite kueleza sera na vipaumbele vyao vya kuwahudumia wananchi .
Rai hiyo ameitoa leo wakati wa Ufunguzi wa kikao cha kamati ZA kampeni ngazi za kata ,Wilaya na mkoa kilichofanyika wilayani Korogwe mkoani hapa na kuwataka kuendelea kuwa waadilifu, kwani wana jukumu kubwa la kutumikia wananchi kwenye maeneo yao.
Amesema kuwa wagombea hao hawatakiwi kuvimba, kwani chama kina imani nao kuwa wataweza kuwa viongozi ambao watafikika kwa ukaribu na haraka badala ya kujiwekea mipaka.
“Twendeni tukakipiganie chama ili kiweze kupata ushindi wa kishindo badala ya kuanza kuvimba na kuwa mtu wa majivuno kwani chama kimekuamini kuwa utaweza kuwa suluhu ya kutatua kero za wananchi kwenye eneo lako,”amesema mwenyekiti huyo.
Alitumia fursa hiyo kuwaonya wanachama wa chama hicho ambao wamejipanga kufanya hujuma kuwa wakibainika watachukuliwa hatua kali za kinidhamu.
Mwenyekiti mstaafu CCM Mkoa wa Tanga, Mussa Shekimweri amesema kuwa ushindi wa chama hicho unategemea kamati za uchaguzi kutimiza wajibu wao kwa ukamilifu wake.
“Chama hiki kipo imara lakini ifikapo kwenye uchaguzi sio jambo jema kudharau, bali tuhakikishe tunajipanga katika kuhakikisha kwenye ngazi zote tunapata kura za kutosha,” amesema Shekimweri.
Mjumbe wa NEC Mkoa wa Tanga, Salum Mohamed Ratco aliwataka wajumbe wa kamati hizo kutoa ushirikiano kwa viongozi ili kuweza kupata ushindi wa kishindo.
PATA HABARI YA WWE MILIKI KIWANJA CHA KIWANDA PAMOJA NA £56,565,656,000 ONLINE LIVE HAPA + UCHAGUZI UKIISHA UTAGAWA KWA WATANZANIA £56,565,656,000 /56,000,000 maana tumekukabidhi NYOTA Yetu YA KUPATA HELA
PAMOJA NA bonanza la “We JuDGE….”
https://youtube.com/shorts/_jB1m_sfFuM?si=wSugXDCDnASW1bK6