Wagombea udiwani 124 CCM wakosa upinzani Arusha

ARUSHA; MSIMAMIZI wa Uchaguzi Mkoa wa Arusha, Apolinary Seiya amesema wagombea wa udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kata 124 kwenye mkoa huo hawana wapinzani.
Seiya amesema Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imepitisha wagombea udiwani katika kata zote 160 za Mkoa wa Arusha.
Alisema mkoa huo una majimbo saba ya uchaguzi na katika kata 36 zilizobaki vyama vya upinzani vimeweka wagombea.
Seiya alisema katika Jimbo la Ngorongoro lenye kata 30, CCM wagombea 28 wa CCM hawana wapinzani.
Alisema katika kata za Oldonyisambu na Sale, Chama cha ACT Wazalendo kimeweka wagombea. Nao ni Kabaney Mojah wa kata ya Oldonyosambu na Mussa Radia wa Sale.
Seiya alisema katika Jimbo la Longido lenye kata 20, INEC imeteua wagombea 20 na wote ni wa CCM.
Alisema katika Jimbo la Monduli lenye kata 20, tume imeteua wagombea 20 na wote ni wa CCM.
Alisema katika Jimbo la Arumeru Mashariki lenye kata 35, imeteua wagombea wa kata 20 wa CCM wasio na wapinzani na kati ya kata 15, vyama vya upinzani vimeweka wagombea.
Seiya alisema katika jimbo la Arusha Mjini wagombea udiwani wa CCM kutoka katika kata tisa kati ya 25 hawana wapinzani.
Alisema katika Jimbo la Karatu, wagombea kupitia CCM katika kata 14 kati ya 22 hawana wapinzani.
Seiya alisema kwenye Jimbo la Arumeru Magharibi, wameteuliwa wagombea 13 wa CCM na hawana wapinzani.
PATA HABARI YA WWE MILIKI KIWANJA CHA KIWANDA PAMOJA NA £56,565,656,000 ONLINE LIVE HAPA + UCHAGUZI UKIISHA UTAGAWA KWA WATANZANIA £56,565,656,000 /56,000,000 maana tumekukabidhi NYOTA Yetu YA KUPATA HELA
PAMOJA NA bonanza la “We JuDGE….”
https://youtube.com/shorts/_jB1m_sfFuM?si=wSugXDCDnASW1bK6
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com