Wagombea udiwani Ngorongoro waomba bajeti kusukuma miradi

NGORONGORO: WAGOMBEA udiwani wa Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha wamesema kuwa bajeti ya maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya hiyo ya Sh bilioni 88 haitoshi kusukuma miradi ya maendeleo katika jimbo.

Hivyo, wameiomba Serikali Kuu kupandisha haidi kufika Sh bilioni 200 angalau iweze kusukumaa miradi.

Madiwani hao wamesema wanasababu nyingi za kuomba bajeti hiyo kufikia kiasi hicho ni kutokana na jiografia na Jimbo la Ngorongoro na bajeti ya zamani imepitwa na wakati kutokana na sensa ya sasa kuwa na wananchi wengi katika jimbo hilo ambao wanahitaji sana huduma za maendeleo.

Madiwani hao walitoa maombi hayo kwa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliokuwa wakifanya mikutano ya kampeni iliyofanyika katika kata za Arashi na Piyaya na kuwaomba kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za afya, elimu, na kupunguza migogoro ya ardhi sambamba na ongezeko la bajeti.

Mgombea udiwani wa kata ya Arash Methew Siloma amewaomba viongozi wa chama kuwasilisha ombi la ongezeko la bajeti katika vikao vya ngazi ya juu vya kichama na kiserikali ili wananchi wa Jimbo la Ngorongoro waweze kunufaika na miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo.

Siloma amesema kuwa pamoja na kuomba ongezeko la bajeti pia wamewaomba viongozi hao wa chama kulipa kipaumbele suala la kutenga eneo la malisho kwa wafugaji kwani kukosekana na eneo hilo ni changamoto kubwa kwa wafugaji kwani wamekuwa wakitangatanga katufa eneo la malisho

Katika mkutano huo, kiongozi wa mila wa jamii ya kimasai maarufu kwa jina la Laigwanani, Konini Martin, ameungana na madiwani juu ya ongezeko la bajeti pamoja na wananchi kwa kuitaka serikali kuzingatia changamoto zinazowakabili wafugaji, huku akieleza matumaini ya jamii hiyo kwa viongozi wa CCM.

Naye, Mgombea ubunge wa Jimbo la Ngorongoro, Yannick Ndoinyo aliungana na madiwani hao juu ya ongezeko la bajeti na kutengwa sehemu ya malisho kwa wafugaji na kusema kuwa hayo yote yatapatiwa ufumbuzi kwa kuwa serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni sikivu na inawajali sana wananchi wake kwa hali na mali.

Wagombea hao wa uwanatarajiwa kuendelea na kampeni katika kata nyingine za Jimbo la Ngorongoro huku wakiahidi kushirikiana na serikali katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button