Wagombea, vyama vizingatie kampeni za kistaarabu kulinda amani ya nchi

LEO (Agosti 28, 2025) ni uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025.
Vyama vya siasa 18 vilivyosaini kanuni za maadili na kuridhia kuingia katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu kuanzia leo vitaanza kunadi ilani na wagombea wake wa nafasi za urais, ubunge, udiwani na uwakilishi kwa Zanzibar.
Kampeni zinazoanza leo zinaashiria nchi inakaribia katika tukio la kihistoria ambalo Watanzania wenye sifa za kuwa katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura watatumia haki yao ya msingi kupiga kura Oktoba 29, 2025 kuchagua viongozi wanaowataka kwa miaka mitano ijayo.
Kipindi cha kampeni kinachoanza leo, kitaisha Oktoba 28 kwa Tanzania Bara na Oktoba 27 kwa Zanzibar ili kupisha upigaji kura ambao ndio kilele cha kampeni zenyewe.
SOMA: Kumekucha kampeni za Uchaguzi Mkuu
Tunavikumbusha vyama vya siasa na wagombea kukumbuka wana dhamana kubwa kuhakikisha amani, utulivu na umoja wa Watanzania unaendelea kuwepo kabla, wakati na baada ya uchaguzi.
Tunu hizo za taifa zitaimarishwa zaidi kipindi hiki cha kampeni kuonesha ukomavu wa wagombea kisiasa na kiutu kwa kufanya kampeni za kistaarabu zenye kuzingatia miiko ya Kitanzania, kanuni, miongozo na sheria za nchi.
Tunatarajia kama nchi ilivyovuka salama katika vipindi cha uchaguzi vilivyopita, na mwaka huu hali itakuwa njema zaidi hasa kutokana na msisitizo uliotolewa na viongozi wa serikali, dini na kijamii kuhusu umuhimu wa kutunza amani.
Taasisi na mamlaka zinazosimamia Uchaguzi Mkuu ikiwemo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) zimekutana na makundi mbalimbali ya wadau wa uchaguzi vikiwemo vyama vya siasa na wagombea, yote hii ni ili kuhakikisha haki na amani vinazingatiwa wakati wa mchakato wa uchaguzi.
Zipo nchi zilizoingia kwenye historia ya machafuko na vurugu kutokana na kushindwa kupima kauli wakati wa kampeni na matokeo yalipotangazwa na kusababisha vifo, uharibifu mkubwa wa mali, chuki na uhasama unaoendelea kujidhihirisha hata sasa.
Tanzania tuna historia ya kuvuka nyakati hizi kwa amani, hivyo tuendeleze historia hii njema, tusivichokoze vyombo vya dola kwa kutotii sheria bila shuruti bali tuoneshe ukomavu kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa.
Tunaamini ukomavu wa wanasiasa wa Tanzania tangu kuanza kwa uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1995 utadhihirika pia sasa.
great
I make $88 an hour to work part time on a laptop. I never thought it was possible but my closest friend easily made $18,000 in 3 weeks with this top offer and she delighted me to join. .Visit the following article for new information on how to access…….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Make money while staying at home and working online. i have just received $35k of my last month working and i was doing this in my part time online. in this new year i can earns more and more and i believe you guys can also can more cash from this job. to join right now follow details on this web.
Open This…. http://Www.CartBlinks.Com
Thank you a lot for sharing this with all folks you really know what you
are speaking about! Bookmarked. Please additionally seek advice from my site =).
We may have a hyperlink trade contract among us
I’ve recently started a site, the info you offer on this site has helped me greatly. Thank you for all of your time & work.