Wagombea, vyama vizingatie kampeni za kistaarabu kulinda amani ya nchi

LEO (Agosti 28, 2025) ni uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025.Vyama vya siasa 18 vilivyosaini kanuni za maadili na kuridhia kuingia katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu kuanzia leo vitaanza kunadi ilani na wagombea wake wa nafasi za urais, ubunge, udiwani na uwakilishi kwa Zanzibar.

Kampeni zinazoanza leo zinaashiria nchi inakaribia katika tukio la kihistoria ambalo Watanzania wenye sifa za kuwa katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura watatumia haki yao ya msingi kupiga kura Oktoba 29, 2025 kuchagua viongozi wanaowataka kwa miaka mitano ijayo. Kipindi cha kampeni kinachoanza leo, kitaisha Oktoba 28 kwa Tanzania Bara na Oktoba 27 kwa Zanzibar ili kupisha upigaji kura ambao ndio kilele cha kampeni zenyewe.

Tunavikumbusha vyama vya siasa na wagombea kukumbuka wana dhamana kubwa kuhakikisha amani, utulivu na umoja wa Watanzania unaendelea kuwepo kabla, wakati na baada ya uchaguzi. Tunu hizo za taifa zitaimarishwa zaidi kipindi hiki cha kampeni kuonesha ukomavu wa wagombea kisiasa na kiutu kwa kufanya kampeni za kistaarabu zenye kuzingatia miiko ya Kitanzania, kanuni, miongozo na sheria za nchi.

Tunatarajia kama nchi ilivyovuka salama katika vipindi cha uchaguzi vilivyopita, na mwaka huu hali itakuwa njema zaidi hasa kutokana na msisitizo uliotolewa na viongozi wa serikali, dini na kijamii kuhusu umuhimu wa kutunza amani. Taasisi na mamlaka zinazosimamia Uchaguzi Mkuu ikiwemo Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) zimekutana na makundi mbalimbali ya wadau wa uchaguzi vikiwemo vyama vya siasa na wagombea, yote hii ni ili kuhakikisha haki na amani vinazingatiwa wakati wa mchakato wa uchaguzi.

 

 

Habari Zifananazo

4 Comments

  1. I just got paid $22k working off my laptop this month!** And if you think that’s cool, my divorced friend has twin toddlers and made over $22620 her first month. details on this website**Want the secret?** Copy this Website and choose HOME TECH OR MEDIA…..

    Here is I started_______ https://Www.CashHive1.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button