Wagombea, wastaafu wamuombea kura Dk Samia

ARUSHA: WAGOMBEA ubunge na wabunge wastaafu wanane wamefika Jimbo la Longido mkoani Arusha kumuombea kura mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa serikali ya chama hicho ndio pekee itakayoleta maendeleo jimboni hapo kwa muda mfupi.
Wagombea hao ni Martha Gido na Chiku Issa wabunge wateule viti maalumu UWT, Lulu Mwacha mbunge mteule UVCCM Mkoa wa Arusha, Issack Joseph mbunge mteule Jimbo la Monduli na Mbunge mwenyeji DkSteven Kiruswa.
Wabunge wastaafu ni pamoja na Lekule Laizer Jimbo la Longido na pia alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha na kwa sasa ni kiongozi wa Milla wa Jamii ya kifugaji ya Kimasai maarufu kwa jina la Laigwainani ,Christopher Ole Sendeka Jimbo la Simanjiro na Zaituni Swai UWT Mkoa wa Arusha.
Lekule aliwaasa viongozi wa milla,viongozi wa chama ngazi ya mabalozi,matawi na kata kuhakikisha wanawahamashisha wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 29 mwaka na kumchagua Rais kwani amefanya mambo makubwa kwa kushirikiana na Mbunge mteule wa Jimbo hilo sambamba na madiwani.
Laigwainani Lekule alisema Rais amepeleka mamilioni ya fedha za miradi katika jimbo la Longido katika kipindi chake cha muda mfupi hivyo fadhila kwa wananchi wa jimbo hilo ni kumpa kura za kishindo ili ajue kuwa jamii ya kifugaji inathamini mchango wake.
Alisema mbali ya hilo mbunge mteule Kiruswa naye anastahili kurudi kwa kishindo kwa kura nyingi kwani ni mbunge msikivu ,mnyenyekevu ,mfuatiliaji na amefanya mambo makubwa katika jimbo la Longido hivyo anastahili kupata kura za kishindo pia.
Naye Sendeka na Swai kwa pamoja waliwakumbusha wananchi wa Longido kuwa Rais Samia ni kiongozi anayejali watu na anatatua changamoto kwa wakati na katika jimbo hilo amefanya mambo makubwa hivyo anastahili kupewa kura nyingi.
Lulu Mwacha ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo aliwakumbusha wananchi wa Longido walipotoka na walipo sasa na kuwataka kulipa fadhila kwa Rais kwani amejitoa kwa hali na mali kwa kupeleka fedha nyingi za miradi ya maendeleo kama vile afya,elimu,maji na barabara kuliko Rais yoyote aliyewahi kuiongoza nchi hii hivyo anastahili kupewa kura za kishindo.
Mwacha alisema zamani huduma ya afya ilikuwa mtihani kwa akina mama wajawazito na huduma ya mama na mtoto pia ilikuwa kitendawili lakini kwa sasa huduma hizo zimesogezwa kila kata katika jimbo la Longido na kupunguza usumbufu kwa akina mama kwenda umbali mrefu kutafuta huduma hiyo ya afya.
‘’Tumpe kura za Kishindo mgombea urais wwa CCM ,tumpe kura za kutosha mgombea ubunge wa jimbo la Longido Kiruswa na tusiwasahau madiwani wa kata zote 20 za Jimbo la Longido kwa pamoja wanapaswa kufanya kazi kama timu kwa maendeleo ya jimbo’’alisema Mwacha
Naye mbunge mteule Monduli,Issack Joseph alisema yeye anahistoria na jimbo la Longido na kusema kuwa jimbo hilo lilipoanzishwa na sasa ni mabadiliko makubwa sana pongezi zote za dhati anapaswa kupewa Rais kwa kuwa amefanya mambo makubwa sana katika miradi ya maendeleo.
Mbunge mteule UWT,Chiku Issa yeye aliwakumbusha wananchini kwa kuwaonyesha mfano wa karatasi ya kupiga kura na kusema kuwa wasifanye makosa kwani mbele ya karatasi hiyo wakiona neon CCM wanapaswa kuwapigia kura Rais,mbunge na madiwani.
Naye Kiruswa alisema kuwa Rais Samia alipeleka fedha za miradi ya maendeleo zaidi ya shilingi bilioni 106 katika jimbo hilo fedha ambazo ni nyingi katika muda mfupi alioongoza nchi hivyo anastahili kulipwa fadhila kwa kupewa kura za kishindo na wananchi wa Longido.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com