Wagonjwa wa kisukari wapungua

TAKWIMU za utafiti na ufuatiliaji wa viashiria hatarishi vya magonjwa yasiyoambukiza uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) mwaka 2024, zinaonesha ugonjwa wa kisukari umepungua kwa asilimia 6.2 kutoka asilimia 9.1 mwaka 2012 hadi asilimia 2.9 mwaka 2023, Bunge limeelezwa.
Akiwasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara ya Afya kwa mwaka 2025/2026, Waziri wa Afya Jenista Mhagama, amesema kuwa pia tatizo la shinikizo la juu la damu limepungua kutoka asilimia 26 mwaka 2012 hadi asilimia 22 mwaka 2023.
“Hali hii inaweza kuwa imechangiwa na kupungua kwa matumizi ya pombe kutoka asilimia 29.3 mwaka 2012 hadi asilimia 20 mwaka 2023 na matumizi ya tumbaku kutoka asilimia 14.1 mwaka 2012 hadi asilimia 10 mwaka 2023,” amesema Waziri Mhagama.
–