Wajadili mikakati uzalishaji miche ya korosho

KITUO cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Naliendele mkoani Mtwara  kimejadili mpango mkakati wa kuzalisha miche bora ya korosho milioni mbili inayotokana na mbegu bora zenye ukinzani dhidi ya ugonjwa wa blaiti ya mikorosho ili kusambaza kwa wakulima.

Akizungumza wakati wa mkutano wa ndani wa kisayansi kuhusu kupitia kazi za utafiti zilizofanyika mwaka 2023/2024, Mkurugenzi wa Kituo cha TARI Naliendele Dk Geradina Mzena amesema lengo la kikao hicho ni kangalia mafanikio, changamoto na kuja na mpango kazi wa kukabiliana na changamoto hizo kwa msimu wa 2024/2025 ili kuwasaidia wakulima kuongeza uzalishaji na tija.

Mkutano  huo umefanyika mkoani Mtwara na kukutanisha watafiti, maofisa kilimo  wa sekretarieti za mikoa na halmashauri mbalimbali zinazozilisha korosho, pamoja na wadau mbalimbali wa korosho.

Hata hivyo mafanikio ya yoliyopatikana katika mwaka huo  2023/2024 kwenye zao hilo ni pamoja kugudua mbegu bora za korosho aina nane zilizotolewa mwezi Julai 2024 kwa kuzitafiti kwa muda wa miaka 12.

“Matarajio ya mkutano mzima ni kujenga uelewa kwamba sasa tutatambua changamoto za wakulima zipo wapi na nini kifanyike,”amesema Mzena

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Juma Yusufu ametoa pongezi wa watafiti wa taasisi hiyo kwa jitihada kubwa zinazochukuliwa katika kufanikisha tafiti mbalimbali.

Hata hivyo kufanikisha ugunduzi wa mbegu bora za korosho zinazostahimili ugonjwa huo wa blaiti kwani hayo ni mafanikio makubwa ambayo yana kila dalili ya kufikia lengo la serikali la kuzalisha tani milioni 1 ifikapo mwaka 2029/2030.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Mshaghulei Ishiki ambaye ni mgeni rasmi katika mkutano huo, amepongeza jitihada za utafiti  zinazofanywa na kituo hicho kwani zinaleta tija kubwa kwa wakulima.

Habari Zifananazo

Back to top button