Wajasiriamali Afrika wahimizwa uwekezaji utalii

WAJASILIAMALI wadogo na kati kutoka barani Afrika wamehimizwa kuwekeza Tanzania hususan sekta ya utalii kwani ndio sekta yenye uhakika wa kipato.

Mbali na kuwahimiza kuwekeza wajasiliamali hao wanawake na vijana wametakiwa kujisajili katika mfumo rasmi wa kifedha ili kutambulika na serikali na benki waweze kukopesheka.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hanspaul, Sathir Singh Hanspaul amesema hayo katika kongamano la tatu la wajasiliamali wanawake na vijana Afrika lililoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali (NGO’S) la Accelerate Afrika Foundation na kuhudhuriwa wanawake na vijana 200 kutoka katika nchi 20 Afrika lililofanyika Arusha.

Advertisement

Hanspaul amesema wakati umefika kwa wajasiliamali hao kufungua kampuni za kitalii ikiwa ni njia pekee ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan aliyefungua milango katika sekta hiyo kwa kuhimiza utalii kufuatia filamu yake ya The Royar Tour.

Amesema sekta ya utalii kwa sasa ina fursa nyingi sana za kujiingizia kipato hivyo ni wakati wa wajasiliamali wadogo na wa kati kujikita katika sekta hiyo ni kuacha zana ya kutaka kuajiriwa serikalini kwani serikali haiwezi kuajili wanawake na vijana wote katika nchi zao.

Mkurugenzi huyo mbali ya kuhimiza hilo aliwataka wajasilimali hao kuhakikisha wanasajiliwa katika mifumo rasmi ya kiserikali na kibenki ili waweze kutambulika na kukopeshwa na benki.

Amesema karne hii sio ya kufanya biashara kiholela ni lazima uwe katika mfumo rasmi wa kiserikali na uwe na nidhamu na matumizi ya fedha katika kibiashara na ukizingatia hayo hakika unaweza kufanikiwa katika maisha bila vikwazo.

Akifungua kongamano hilo, Mratibu Mkuu wa NGO’S ya Accelerate Afrika Foundation, Pendo Lema amesema changamoto nyingi zinawakabili wajasiliamali wanawakee na vijana katika kufanya biashara ikiwa ni pamoja na kukosa mtaji wa biashara na wanafanya biashara bila kusajiliwa na taasisi za kiserikali hivyo kushindwa kutambulika serikalini na taasisi za kifedha.

Lema amesema kufuatia hali hiyo wameamua kuwakusanya wajasiliamali katika nchi hizo za Afrika ili kuwapa elimu ya umuhimu wa kujisajili serikalini na wakifanya hivyo ni rahisi kukopesheka katika taasisi za kifedha kwani hakuna mfanyabiashara aliyetoka kimaisha bila kukopa benki.

Naye Kyenekiki Kyando mwakili kutoka taasisi ya Bima ya Sanlam aliwahimiza wajasiliamali kuhakikisha wanakuwa nabBima katika biashara zao kwani zinaweza kuwasaidia katika majanga mbalimbali ikiwemo moto.