Wakazi Dar kufanyiwa uchunguzi magonjwa yasiyoambukiza

DAR ES SALAAM: Wakazi wa Dar es Salaam watapata nafasi ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu bure kwa magonjwa yasiyoambukiza katika kambi maalumu itakayofanyika Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Kambi hiyo ya siku mbili itakayoanza Novemba 28-30, 2025, imeandaliwa na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana kwa kushirikiana na Taasisi ya GSM
Foundation.

Huduma zitakazotolewa katika kambi hiyo ni pamoja na uchunguzi na matibabu
ya kisukari, shinikizo la juu la damu, macho, pua koo na masikio, afya ya kinywa na meno.
Pia magoniwa ya ndani, magonjwa ya wanawake na afya ya uzazi, ngozi, huduma za radiolojia pamoja na Bima za Afya kwa watu wasio na uwezo.
Akizungumza Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana Dk, Jumanne Mafele amesema magonjwa yasiyoambukiza yanaongoza kwa
vifo, hivyo ni muhimu wananchi kutumia fursa hiyo.

“Takwimu za Shirika la Afya Duniani zinaonesha kuwa magoniwa yasiyoambukiza yanazidi kuongezeka kwa kasi hivyo ni muhimu wananchi kujenga utamaduni wa kufanya uchunguzi wa afya zao mara kwa mara ili kuchukua hatua mapema,”amesema Dk Mafele.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya GSM Foundation, Faith Gugu amesema kuwa lengo la kambi hivo ni kuwafikia watu 1000 ambapo kati ya watu 300 watakaobainika kuwa na matatizo na wasiokuwa na uwezo watapatiwa Bima za Afya bila malipo na watakao pewa kipaumbele ni watoto, wanawake na wazee.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com