Waliohusika upotevu wa fedha AMCOS wachukuliwa hatua

SERIKALI ya Mkoa wa Mtwara imesema viongozi wa vyama vya msingi 17 (AMCOS) waliohusika na upotevu wa korosho za wakulima na wengine kufanya udanganyifu kwenye malipo wamechukuliwa hatua za kisheria na baadhi yao kuanza kurejesha fedha hizo.

Hayo yamejiri wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara kuhusu kutoa taarifa za utekelezaji wa Ilani pamoja na changamoto zilizojitokeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo na jamii kwa ujumla kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2025.

Taarifa hiyo ya utekelezaji wa Ilani imewasilishwa na Mkuu wa Mkowa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ambapo moja ya changamoto iliyojitokeza kwenye taarifa na kuibua malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho ni pamoja na upotevu wa korosho na malipo pungufu wanayolipwa wakulima wa zao hilo.

Baadhi ya viongozi hao akiwemo Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Mtwara Vijijini, Nashir Mfaume amesema baada ya kujiridhisha na taarifa hiyo amegundua kuwa changamoto kubwa iko kwa Amcos zao.

‘’Kati ya maadhimio tuliyoyatoa kwenye halmashauri kuu ya wilaya tumeagiza kwamba vyama vyote zilivyopoteza korosho na kuwaibia wakulima vichukuliwe hatua wakiwemo viongozi wenyewe wa Amcos’’

Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Tandahimba, Isamail Mkadimba amesema msimu wa kilimo wa mwaka 2024/2025 kumekuwa na changamoto ya kukosewa kwa majina ya wakulima wa zao hilo kuliko misimu iliyopita pamoja na upotevu wa korosho nyingi za wakulima kwa baadhi ya Amcos.

Hata hivyo amewashauri wajumbe wa kikoa hicho kuridhia taarifa ya iliyotolewa na mkuu huyo wa mkoa juu ya changamoto hiyo kwa kuruhu serikali ya mkoa na wilaya kwa ujumla kulifanyia kazi jambo hilo.

Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Mtwara, Grace Masambaji amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya upotevu wa korosho kwa baadhi ya Amcos na kwamba hatua zimeanza kuchukuliwa huku baadhi ya Amcos zimeanza kurejesha fedha hizo.

Kwa upande wake Mkuu huyo wa mkoa amesema serikali tayari imeanza kuchukua hatua dhidi ya wahusika huku akimuomba mwenyekiti wa Ccm mkoa wa Mtwara kuruhusu hatua zaidi zichukuliwe ili iwe fundisho kwa wangine.

‘’Uchumi wetu mkubwa sisi wana mtwara ni korosho ila kuna watu wanatuharibia hili zao, kuna malalamiko mengi sana kwenye zao la korosho wote tunafahamu pamoja na kucheleweshewa baadhi ya malipo lakini mengine yanatengenezwa na viongozi wetu wa hivi vyama vidogo vya Amcos siyo kwa bahati mbaya’’amesema Sawala

Habari Zifananazo

Back to top button