MWAKILISHI kutoka ubalozi wa Sweden (SIDA) Stephen Chimalo amesema wanataka uwepo mfumo mzuri kupitia wadau na serikali kuhakikisha waandishi wa habari wanakuwa kwenye mazingira salama ya utendaji kazi.
Chimalo amesema hayo leo Novemba 2, 2024 katika maadhimisho ya siku ya kupinga dhuluma na ukatili dhidi ya waandishi wa habari ambapo amesema waandishi wa habari wamekuwa wakishindwa kufanya vizuri kuripoti kero na changamoto kutokana na kukosa ulinzi.
“Mwandishi wa habari anapotaka kufanya kazi yake ahakikishiwe usalama wake wa kimazingira na kiafya na sio Tanzania pekee hata nchi nyingine waandishi wanahatarishiwa usalama wao hivyo tunataka uwepo mifumo mzuri ambayo inaweza kujengwa kwa kupitia wadau na serikali kwa kuhakikisha waandishi wanakuwa kwenye mazingira yaliyosalama,”amesema Chimalo.
Chimalo amesema kuna mwandishi mmoja wa kike kutoka mkoani Manyara alikuwa anafanya utafiti kuhusu wadada wanao jiuza nyakati za usiku alijiuliza katika usalama wa mwandishi huyu pia mwingine alikuwa anataka kuripoti habari kuhusu mtoto mchanga kutupwa lakini wanakijiji walidai asiandike hiyo ni changamoto.
“Napenda kuwashukuru UTPC na IMS kuhakikisha wanatekeleza jambo la usalama kwa waandishi na kujenga usalama kati ya jeshi la polisi na Waandishi wa habari kwa juhudi wanazozifanya ikiwemo kuwalinda na kuwathamamini waandishi wa habari”amesema Chimalo.
Huyu Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo
Chimalo amesema Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu,Sayansi na Utamaduni (UNESCO) imeanza kufanya mchakato na Mfuko wa taifa wa bima ya Afya (NHIF )kuhakikisha waandishi wa habari wanapata bima za afya lengo kuwahakikishia usalama wao kiafya.
‘Tunaweza kuwashawishi zaidi kusaidia waandishi kupata bima za afya,usalama wa waandishi pamoja na kupata kipato, ukiwa na uhakika wa mapato hata uhakika wa kule unakoenda kutafuta habari unakuwa na usalama na hili ni kipaumbele sababu ya usalama wa waandishi”Chimalo.
Siku hii ni kubwa kwetu kutokana na siku hii ambapo waandishi wawili wa Ufaransa waliuwawa na kupelekea tarehe 2 Novemba iwe inaadhimishwa lengo kukumbusha uwajibikaji kwa serikali kuhakikisha uwepo wa Usalama wa Waandishi.
Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) Deogratius Nsokolo amesema katika kipindi Cha mwaka 2024 ambapo UTPC wamerekodi jumla ya matukio 14 yakihusisha waandishi wa habari 26 Kati ya hao 21 ni Wanaume na watano ni wanawake.
“Wahusika wa matukio hayo ya ukiukwaji wa haki za waandishi wa habari wamekuwa wakiachwa bila kuchukuliwa hatua ,ukosefu huu wa uwajibikaji wa adhabu imejenga mazingira ya hofu na kujidhibiti hali hii imedhoofisha uwezo wa vyombo vya habari kufanyakazi kwa Uhuru na hivyo kudidimiza demokrasia”amesema Nsokolo.
Edwin Soko akiwasilisha mada inayohusu Impunity and Impact to Journalism in Tanzania amesema madhila kwa waandishi wa habari hapa nchini kuanzia Januari hadi sasa vipo visa mkasa 22 ambavyo vimekwisha tokea hivyo wasipuuze katika ulinzi na usalama wao.
“ Kwa mujibu wa Shirika la UNESCO limetoa takwimu kwa mwaka 2022 kuwa hapa duniani hasa kwenye nchi zinazoendelea na vita na migogoro waandishi 28 walipoteza maisha na mwaka 2023 waandishi wa habari 38 walipoteza Maisha na mwaka huu takwimu bado haijatolewa hali itakuwaje inaweza pia kuongezeka “amesema Soko.
“Sasa hivi Mitandao ya kijamii inachukua nafasi k ubwa katika vyombo vya habari vingine ambapo vyombo hivyo kumejengeka hofu na woga na matokeo ya kubadilisha maudhui na jamii kuanza kukosa uaminifu kupitia vyombo hivyo”amesema Soko.