WANANCHI 50 kati ya 599 kutoka vijiji vinne vilivyopo Kata ya Engaruka wilayani Monduli wameanza kulipwa fidia ya Sh bilioni 6.2 kati ya Sh bilioni 14.4 kwa ajili ya kupisha mradi wa magadi soda.
Fidia hiyo ya Sh bilioni 6.2 kati ya Sh bilioni 14.4 inalipwa katika vijiji vinne vya Engaruka Chini, Mbaash, Idonyonado na Irerendeni wana bilioni 14.4 huku fedha zingine zilizobaki zikienda katika shughuli mbalimbali za miradi ya maendeleo huku akisisitiza ndani ya siku 90 wananchi hao wanaanza kulipwa fidia wataondoka eneo husika ili kupisha uwekezaji.
Akizungumza na wananchi eneo la Engaruka wilayani Monduli mkoani Arusha kwa niaba ya Rais Samia Hassan Suluhu katika uzinduzi wa zoezi la ugawaji fidia ,Waziri wa Viwanda na Biashara,Dk Seleman Jafo alisema fedha hizo zimetolewa na Rais Samia Hassan Suluhu ikiwa ni mkakati wa kuendeleza miradi kimkakati yenye tija kwa Taifa.
Amesema mchakato wote wa ulipaji fidia hiyo utaratibu wake usizidi Februari 15 mwaka huu lakini pia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC ) wafuatilie malalamiko yote ya wananchi juu ya ulipwaji fidia hiyo na kuongeza kuwa mradi huo wa Engaruka wawekezaji mbalimbali wamejitokeza kutaka kuja kuwekeza eneo hilo
Amesisitiza wawekezaji hao wasiwe makanjanja bali wawe ni wawekezaji wenye tija na kuleta manufaa kwa nchi na wananchi husika ikiwemo uchumi kukua kutokana na malighafi hii muhimu kupatikana nchini ikiwemo upatikanaji wa malighafi mzuri kutoka Tanzania