Wananchi Kagera wamuombea Rais Samia

MKUU wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa ameungana na viongozi wa dini zote kufanya maombi kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan, taifa na viongozi wake.
Maombi hayo ya pamoja yamefanyika uwanja wa Kaitaba kama sehemu ya ratiba ya tamasha la Ijuka Omuka (Make Kagera Great Again)ambalo limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera na wadau wa maendeleo wanaoishi ndani na nje ya nchi.
Tamasha hilo linalenga kuibua fursa za uwekezaji zilizozojificha ambazo zitaunganisha mawazo ya wadau na wabobezi tofauti wa kiuchumi wenye muono wa kuuweka mkoa wa Kagera katika nafasi za juu za kiuchumi.
Wananchi wengi wamekusanyika katika uwanja huo ambapo licha ya kumuombea afya njema Rais bado wameomba kila mdau anayetoka mkoa wa Kagera na akafanikiwa arudishe shukurani nyumbani na kuwekeza tena Kagera na kuwa wamechoka kuuuona mkoa huo ukiwa katika viwango vya chini vya uchumi.
Tamasha Hilo litaendelea hadi Desemba 26. Kesho Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko atawaunganisha wakazi wa Kagera katika kikao cha pamoja cha uwekezaji.