Wananchi Kishenge waliridhia ujenzi eneo la biashara

BUKOBA: Katika kutekeleza miradi ya maendeleo, Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kupitia timu ya uratibu wa kuhamisha makaburi ya Kishenge imekutana na wananchi wanaodhaniwa kuwa ndugu wa marehemu waliolazwa kwenye makaburi hayo, kwa ajili ya majadiliano ya pamoja ya utekelezaji wa mradi huo.

Kikao hicho kililenga kuwafahamisha wananchi hao kuhusu mpango wa Serikali, kupitia ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa wa kutwaa eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa soko kubwa litakaloweza kuhudumia wafanyabiashara,machinga na wajasiliamali wadogo wadogo zaidi ya 2,000.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Jacob Nkwera, amesema kuwa Manispaa ya Bukoba ilipata nafasi ya kuandaa maandiko ya kuomba fedha za miradi, na sasa serikali imeidhinisha fedha zinazokadiliwa kufikia Sh bilioni 9 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

“Tumeidhinishiwa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa complex kubwa, mji wetu ni mdogo na maeneo mengi yamebana, ndio maana tukaamua kuomba kutumia eneo hili la Kishenge tunachoomba ndugu ambao tayari mmehifadhi miili ya marehemu mtuelewe na  tuufanye mji wetu kuwa na maendeleo na kuwafanya wafanyabiaashara kuwa pamoja kufanya biashara zao bila buhudha,”alisema Nkwera .”

Aidha, aliongeza kuwa pamoja na matangazo yaliyotolewa kupitia mitaani na vyombo vya habari, lisingekuwa jambo la busara kuanza mchakato bila kuzungumza na wananchi ambao ni wahusika muhimu.

Kwa kauli moja, wananchi walioridhia mchakato huo waliitaka Halmashauri kuendelea  na utekelezaji wa mradi  huku wakisisitiza umuhimu wa kushirikishwa katika kila hatua ya utekelezaji.

Kwa Mujibu wa mkurugenzi huyo halmashauri tayari imeandika na kutuma nyaraka kwenye ofisi ya Waziri wa Ardhi na Februari 11 mwaka huu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Deogratias Ndejembi ambaye  alitembelea eneo hilo kujionea hali kabla ya kutoa kibali cha kuhamisha makaburi yanatarajiwa kuhamishiwa kwenye kiwanja kilichopimwa, kilichopo Kata ya Buhembe.

Mji wa Bukoba tunakunbana na changamoto ya Machinga na wafanyabiashara kupanga bidhaa chini  pembezeno mwa mji  huku kwa muda mrefu  changamoto ya kukosa eneo la kufanyia biashara ikitajwa mradi huo unaweza kuwa mkombozi kwa Machinga na kuchangia mapato ya ndani kwa Manispaa ya Bukoba endapo wafanyabiashara watakuwa na eneo rasmi  la kufanyia biashara zao.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button