Wananchi kujengewa wodi kituo cha afya Mirerani

KITUO cha afya Mirerani kina changamoto ya upungufu wa wodi ya wanawake na watoto na kusababisha msongamano mkubwa kwa wagonjwa wanapolazwa kwani kinahudumia baadhi ya watu wa wilaya za Simanjiro mkoani Manyara, Arumeru pamoja na mkoani Kilimanjaro.

Mdau wa maendeleo wa Simanjiro, Sporah Mwakipesile kupitia kampuni ya Chusa Mining LTD, ametoa ahadi ya  kujenga wodi mpya ya wanawake, watoto na ofisi ya madaktari na kuboresha mazingira ya mochwari katika  kituo cha afya Mirerani kilichopo katika Kata ya Endiamtu wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Sporah amesema ameamua kufanya hivyo, baada ya kutembelea kituo cha afya Mirerani na kusikiliza changamoto za upungufu wa wodi ya wanawake, watoto na ofisi ya madaktari.

“Mimi na familia yangu ya Chusa Mining Limited tumejipanga kujenga na kukabidhi wodi mbili za au na mama, watoto, Ofisi ya Madaktari, kuboresha mochwari na kwa sababu familia yangu  inafanya shughuli za uchimbaji madini ya Tanzanite Mji Mdogo wa Mirerani ni vyema kuchangia huduma za afya ili ziboreshwe zaidi ukilingamisha na hali ilivyo sasa,mhatutoi pesa hapana tunajenga na tutakuja kukabidhi na kazi itaanza jumatatu,” amesema Sporah.

Nje ya hilo pia  ametembelea kuona changamoto mbalimbali zinazoikabili Shule ya Msingi ya Songambele ya watoto wenye uhitaji maalum na kuchangia vitanda 60, magodoro 120 na viti mwendo 10 kwa watoto wenye ulemavu katika shule hiyo.

“Ili kuniunga mkono ninaomba na nyie ndugu zangu mtuunge mkono isionekqne sisi tuwe tumetoa kila kitu haitapendezakatika sadaka hii tuchangieni kwa pamoja mashuka ila hayo mwingine kampuni yetu ya Chusa Mining LTD itachangia katika kuboresha huduma hizo na ujenzi wa wodi hizo mbili  na vingine hivyo, hivyo unaanza jumatatu ijayo,” amesema Sporah.

Kufuatia hilo Diwani wa Kata ya Endiamtu Lukas Zacharia Chimba aliendesha harambee ya ununuzi wa mashuka katika shule maalum ya Songambele na kupatikana jumla ya Sh milioni 3.6, huku familia ya Diwani wa Kata ya Mirerani Salome Mnyawi ikichangia Sh milioni 5.

Mkurugenzi wa shule ya awali na msingi Glisten ya Mji Mdogo wa Mirerani, Justin Nyari ameunga mkono hafla hiyo kwa kutoa Sh milioni 1 ili kununua mashuka ya watoto wa mahitaji maalum Shule ya Msingi Songambele.

Nyari amesema anaiunga mkono serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna inayofanikisha maendeleo ya sekta mbalimbali kwa jamii.

Ofisa Maendeleo ya Jamii Mji Mdogo wa Mirerani, Floriana Mcharo amesema siku hiyo ya wanawake duniani imekuwa na baraka kwa jamii kutokana na hatua zilizofanywa za kuisaidia jamii Katika sekta ya Afya

Mkazi wa Mji Mdogo wa Mirerani, Peris Mwanyika ambaye amechangia Sh milioni 1 amesema ni vyema kuchangia jamii ili huduma kwa watu zizidi kuboreshwa.

Hata hivyo Naye Mganga wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Dk Lengai Edward ameishukuru kampuni ya Chusa Mining LTD, kwa kuiunga mkono serikali na kuboresha huduma za afya katika kituo cha afya Mirerani, hakika Kwa kufanya hivi mtakua mmeboresha mazingira ya kutolea na kupokea huduma Sasa yanakwenda kuboreka

Dk Edward amesema kituo cha afya Mirerani kina changamoto ya upungufu wa wodi ya wanawake na watoto kutokana na msongamano wa wagonjwa kwani kinahudumia baadhi ya watu wa wilaya za Simanjiro mkoani Manyara na Arumeru mkoani Arusha.

“Kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro tunawashukuru kampuni ya Chusa Mining LTD, kwa kufanya jambo hili jema,” amesema Dk Edward.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button