Wananchi Longido waitwa kupiga kura Oktoba 29

LONGIDO: MGOMBEA ubunge wa Viti Maalum kupitia Jumuiaya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) Vijana, Lulu Mwacha amewaomba wananchi wa Kata ya Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura Oktoba 29.

Aidha, amewaomba wananchi hao kumpa kura za kishindo, Rais Samia Suluhu Hassan kwa ikiwa ni fadhila kwake kwa kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo hilo.

Mwacha alisema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mundarara ulioshirikisha wagombea ubunge wengi  Arusha akiwemo Mgombea Ubunge Jimbo la Monduli, Isack Joseph, wagombe ubunge Viti Maalum UWT, Chiku Issa, Zaitun Swai mgombea ambaye kura zake hazijatosha na Martha Gido na mgombea Ubunge wa Jimbo la Longido Dk Steven Kiruswa.

Alisema shukurani pekee kwa mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan ni kumpa kura za kishindo kwa kuwa amefanya mambo makubwa katika miradi ya maendeleo ikiwemo afya, maji, elimu na barabara kwani miradi hiyo mikubwa haijawahi kuletwa katika jimbo hilo tangu kuanzishwa kwake.

‘’Naomba mjitokeze siku ya kupiga kura na pili mpeni kura za kishindo Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa ameleta miradi mikubwa ya maendeleo katika Jimbo la Longido haijawahi kuletwa miradi hiyo toka kuanzishwa kwa Jimbo la Longido’’alisema Mwacha.

Akimzungumzia mgombea ubunge Jimbo la Longido, Mwacha alisema Kiruswa ni mgombea ubunge msikivu, mnyenyekevu, mcha Mungu na anayesikiliza kila mtu na hana majivuno hivyo anastahili kupewa ubunge kwa mara nyingine ili aweze kuliendeleza jimbo hilo ambalo amelitoa katika mazingira magumu kimaendeleo.

Mwacha alisema Kiruswa ni jembe na ni mfuatiliani katika masuala yote ya maendeleo katika Jimbo la Longido akiwa bungeni na serikalini hivyo shukrani pekee ni kumpa kura za kimbunga na za kishindo ili aweze kuendeleza alipoachia kwa maslahi ya wananchi wa Jimbo la Longido.

Naye Kiruswa katika mkutano huo wa hadhara alisema yeye ni Mbunge wa vitendo na ana kila sababu ya kuomba tena kura ili aweze kuwa mbunge wa Jimbo la Longido kwa kuwa bado ana hamu ya kuifanya Longido kuwa na maendeleo ya kutosha kwani serikali imetimiza kwa asilimia mia miradi mingi ya maendeleo katika Jimbo hilo ikisimamiwa na yeye kwa kila kata.

Kiruswa alisema mbali ya yeye kumpa kura ya ubunge pia aliwaomba wananchi kumpa kura mgombea Urais wa CCM ,Rais Samia Suluhu Hassan ili awe kumalizia miradi iliyobaki katika Jimbo hilo ikiwemo afya, elimu, maji na barabara.

Mgombea ubunge wa Monduli Isack Joseph na Mgombea ubunge wa viti maalumu UWT Mkoa wa Arusha,Chiku Issa mbali ya kumnadi Kiruswa kwa wananchi ili apate kura  kuwa Mbunge wa Jimbo la Longido pia wananchi hao waliombwa kuacha kutompa kura mgombea Rais wa CCM kwani hana shida na wananchi wa Jimbo hilo.

Walisema Kiruswa hana shida na mtu na ni mbunge msikivu asiyekuwa na majivuno hivyo anastahili kura nyingi sambamba na Rais kwani wote wanasifa zinazofanana na wanawajali wananchi katika kuwaletea maendeleo.

Joseph alisema Kiruswa amelitoa Jimbo la Longido mbali na yeye ni shahidi na haoni ni kwa nini wananchi wa Jimbo hilo wasompe kura yeye na Rais kwani wote kwa kushirikiana wamefanya malubwa sana kwa ajilo ya wananchi.

Habari Zifananazo

3 Comments

    1. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
      .
      M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button