Wananchi tushiriki kampeni kubaini wagombea bora

KAMPENI za wagombea nafasi ya urais, ubunge na udiwani katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 zinaendelea nchini. Vyama 18 vimesimamisha wagombea wa nafasi tajwa na baadhi na vimeshazindua kampeni hivyo vinaendelea kunadi sera zao kwenye maeneo mbalimbali.

Hii ni hatua muhimu kuelekea siku ya kupiga kura hivyo huu ni wakati wa wananchi kujitokeza kwenda kusikiliza sera na ahadi za wagombea hao ili kuona ukweli wake kama zinatekelezeka au la ili ifikapo Oktoba 29 wawapigie kura wale wanaoona watawaletea maendeleo ya kweli.

Kipindi hiki cha kampeni ndicho sahihi kwa wananchi kuhudhuria mikutano hiyo ya wagombea, kusikiliza sera na hoja zao na ahadi wanazotoa na kuzipima iwapo zina mashiko na wao kufanya uamuzi siku ya kupiga kura. SOMA: Sheria yatoa mwongozo kampeni za Uchaguzi Mkuu

Ni vyema wananchi kushiriki kwa sababu ni fursa ya kujua chama au mgombea anayenadi sera zinazowalenga wananchi katika maeneo yao na hivyo kumuunga mkono. Kipindi hiki ni muhimu hivyo wananchi wasikubali kutumika na wagombea ama kwa kuwalaghai kwa kuwapa rushwa, zawadi ndogondogo ambazo zitawagharimu miaka mitano ijayo.

Ikumbukwe kuwa maendeleo ya jimbo, taifa au kata miaka mitano ijayo, yanatokana na uchaguzi huo, hivyo ni vyema wananchi tukashiriki katika kampeni ili kusikiliza hoja za wagombea hao kwa sababu ndizo zitakazotoa hatma ya miaka hiyo mitano .

Lakini jambo la msingi pia ni kuangalia kama katika vyama hivyo sera zinaitambua Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050. Tusikubali kuahidiwa kwa maneno bali tuangalie mambo ya msingi wanayonadi kwa sababu wapo wanaoweza kusema wakipewa dola watawanunulia kila mwananchi gari la kutembelea.

Huo ni mfano tu ambao kwa hali ya kawaida haiwezekani kutimiza hilo kwa Watanzania zaidi ya milioni 60. Hivyo ahadi kama hizo ambazo kwa macho zinaonekana wazi hazitekelezeki, wananchi msikubali kudanganywa nazo bali tuwe macho kubaini hayo na kuwakataa wagombea kama hao wenye kutoa ahadi ambazo kwa macho ya kawaida hazitekelezeki.

Bali tuangalie mambo ya msingi ambayo yananadiwa na kwa macho yanaonekana yanatekelezeka. Tuangalie uzalendo wa wagombea na siku ikifika uamuzi wa busara utumike kuwachagua viongozi watakaowavusha kwa miaka mitano ijayo.

Habari Zifananazo

4 Comments

    1. I make $88 an hour to work part time on a laptop. I never thought it was possible but my closest friend easily made $18,000 in 3 weeks with this top offer and she delighted me to join. .Visit the following article for new information on how to access…….
      .
      HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  1. Burkina Faso bans homosexuality as a crime punishable with prison, fines

    In the new law, those found guilty of homosexuality could face a two- to five- year prison sentence.

    Burkina Faso President Ibrahim Traore.
    Burkina Faso President Ibrahim Traore arrives to the Grand Kremlin Palace in Moscow, Russia, on May 10, 2025 [Stanislav Krasilnikov/RIA Novosti via AP]

    Published On 2 Sep 2025
    2 Sep 2025

  2. Burkina Faso bans homosexuality as a crime punishable with prison, fines

    In the new law, those found guilty of homosexuality could face a two- to five- year prison sentence.

    Burkina Faso President Ibrahim Traore.
    Burkina Faso President Ibrahim Traore arrives to the Grand Kremlin Palace in Moscow, Russia, on May 10, 2025 [Stanislav Krasilnikov/RIA Novosti via AP]
    Published On 2 Sep 2025
    2 Sep 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button