Wananchi wa Katembe Mwaloni wafurahia barabara

KAGERA: Ujenzi wa barabara ya lami ya Katembe -Mwaloni inayounganisha Barabara Kuu kutoka nchi za Uganda ,Rwanda na Burundi katika Wilaya ya Muleba mkoani kagera uliogharimu zaidi ya Sh milioni 400 umeleta afueni kwa wakazi wa eneo hilo pamoja na wafanyabiashara wa samaki kutoka katika visiwa vilivyopo ndani ya Ziwa Victoria kwenda ndani na nje ya nchi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ismail Ussi ameridhishwa na viwango vya mradi huo na kuwapongeza Tarura kwa utekelezaji wa mradi wenye viwango ambao unaendeleaa kuwasaidia wananchi.

Alisema kuwa Ili wanachi wapate huduma bora na nguvu ya kuzalisha wanahitaji barabara nzuri zenye viwango na kupitia umma wa wananchi ameshukuru usimamizi wa mradi huo na namna Halmashauri ya Muleba ulivyotoa mapato ya ndani kujenga barabara imara.
Meneja wa Tarura Muleba. Dativa Semforiani akitia taarifa ya mradi wa Barabara ya Katembe Mwaloni alisema uwepo barabara hii umekuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na kuongeza Pato la Muleba.

Alisema barabara iliyozinduliwa leo kwa kiwango cha lami ni km 0.5 ambapo ni kiunganishi kikuu cha wananchi wa eneo hilo na wafanyabiashara wa Rwanda ,Burundi Uganda na Congo hasa wale wanaonunua mazao ya dagaa na samaki.



