Wananchi wa Mabira wafurahia ujenzi barabara

KAGERA: WANANCHI wa kata ya Mabira, iliyopo Wilaya ya Kyerwa Mkoa wa Kagera wameipongeza serikali kwa kuanza ujenzi wa barabara ya Nkwenda- Mabira kwa kiwango cha lami.

Aidha, wamedai kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaongeza ununuzi na kurahisisha usafirishaji wa mazao.

Mwenge wa Uhuru mwaka 2025, umeweka Jiwe la Msingi katika barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 1.0 barabara inayotarajia kukamilika September mwaka huu.

Ramadhan Robert na Bosco Gabriel wakazi wa kata ya Mabila wamesema wamekuwa wakikutana na athari za vumbi na mali zao kuchafuka hali inayopekelekea kukosa soko hasa mazao yakiwa na vumbi.

Meneja wa TARURA, Wilaya ya Kyerwa, Yezron mbasha amesema kuwa mradi huo umegharimu Sh milioni 471.3 fedha ya serikali.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ussi amewataka wananchi kutunza na kulinda miradi hiyo huku akiipongeza TARURA kwa kutekeleza miradi yenye viwango  na yenye ubora ikiwa ni pamoja kuongeza kasi ya upatikanaji wa barabara za lami katika vijiji na maeneo yanayokua kwa kasi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button