Wananchi wanaoishi pembezoni mwa Bukoba kupata maji safi

BUKOBA: Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bukoba (BUWASA) imekamilisha utekelezaji wa mradi wa maji ambao wa Sh bilioni 3.1 utakaonufaisha wananchi zaidi ya 18,000 wa kata tano za Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Mratibu wa Mradi, huo Daudi Byeyanga akitoa taarifa ya kukamilika kwa mradi mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, amesema kuwa mradi ulianza kutekelezwa mwaka 2020 ambapo hadi sasa umekamilika kwa asilimia 100.

Amesema huo ni mradi ambao unaenda kuondoa changamoto kwa wananchi wa kata za pembezoni mwa Mji wa Bukoba ambazo zilipata maji kwa mgao na kata nyingine kutoka Halmashauri ya Bukoba ikiwemo kata Kahororo, Buhembe Nshambya, Kashai na Nyakato.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ussi amewataka wananchi kutunza miundombinu ya miradi ya maji na vyanzo vya maji Ili miradi hiyo iweze kudumu muda mrefu.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button