Wananchi washauriwa kuwa karibu na polisi

DAR ES SALAAM: WITO umetolewa kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili liweze kutekeleza kikamilifu majukumu yake ya ulinzi wa raia na mali zao na kuwezesha utekelezaji wa shughuli za kiuchumi kufanyika kwa amani na salama.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 Ismail Alli Ussi alisema hayo akizindua kituo cha polisi cha Nyamnyusi katika halmashauriya wilaya Kasulu mkoani Kigoma na kubainisha kuwa jeshi la polisi linapaswa kuungwa mkono kuweza kutimiza majukumu yake.

Katika hilo alisema kuwa ni lazima wananchi watoe taarifa katika kufichua mambo ya uhalifu lakini pia kulitumia jeshi la polisi katika migogoro ya shughuli za kijamii sambamba na kuomba ulinzi wanapokuwa na shughuli zao.

Awali Mkuu wa wilaya Kasulu, Isack Mwakisu alisema kuwa mradi huo umejengwa kutokana na mapato ya ndani ya halmashauri na hiyo inatokana na uhitaji wa halmashauri ambayo imemamliza mradi wake wa jengo la utawala hivyo kuona ulazima wa kuwepo kwa ulinzi madhubuti wa rasilimali za serikali, watumishi, wananchi na mali zao.

Akitoa taarifa kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri ya wilaya Kasulu, Msakila Laurent alisema kuwa kiasi cha Sh milioni 114.4 zimetumika kutekeleza mradi huo kutokana na umuhimu wa ulinzi na usalama katika eneo hilo

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button