Wananchi wasifu wanawake wengi kugombea ubunge Mara

MARA : WANANCHI katika Mkoa wa Mara wamepongeza juhudi za uwepo wa usawa uliowezesha kuteuliwa kwa wanawake kugombea nafasi hasa ya ubunge.

Hata hivyo, wamewataka wagombea hao kuleta maendeleo yanayotarajiwa na wananchi badala ya ahadi zao kuishia majukwaani wakati huu wa kampeni. Jimbo la Serengeti lina mgombea kupitia CHAUMMA, Catherine Ruge na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mary Daniel.

“Kama atashinda wa chama tawala, tunatarajia aendelee kuwa mstari wa mbele kuhimiza ajenda ya maendeleo shirikishi kwa wakulima vijijini,” alisema Elizebeth Msilanga akizungumza na HabariLEO juzi. SOMA: Samia apongeza walioteuliwa kugombea

Kwa Musoma Mjini, wagombea wote wawili, Mgore Miraji wa CCM na Angel Lema wa CHAUMMA kwa nyakati tofauti, wameahidi kusimamia uboreshaji wa miundombinu, huduma za kijamii, na uanzishaji wa miradi ya kiuchumi.

Aidha, wameahidi kushirikiana na wananchi kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo. Mkazi wa Musoma, Elisha Kichere alisema ni matumaini yao ni kwamba malengo hayo yatatekelezwa na yeyote atakayechukua jimbo. Kwa upande wa Jimbo la Bunda, wananchi wanategemea kasi ya maendeleo katika sekta za elimu, afya, ajira kwa vijana na michezo mambo ambayo mgombea wa CCM, Ester Bulaya ameahidi kuyafanikisha.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button