Wananchi watakiwa kuhifadhi miradi ya barabara

KAGERA: WANANCHI wanaoishi maeneo yanayopita miradi ya barabara mkoani Kagera wametakiwa kulinda na kuhifadhi miradi ya barabara kwa kuacha tabia ya kutupa uchafu kwenye mitaro.
Wito huo umetolewa leo September 9, 2025 na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Ussi wakati wa uwekaji Jiwe la Msingi katika barabara ya Ihungo yenye kilometa 1.25 yenye thamani ya Sh milioni 506.4 ambayo inaunganisha kata za Kashai na Shambya.

“Kumekuwa na tabia ya uchafuzi wa mazingira kwa barabara zinazopita karibu na makazi yenu, mtu anakusaya taka anatupa katika mitaro mvua ikinyesha itasafirisha uchafu hii haikubariki na imeharibu barabara nyingi,”amesema Ussi.
Ameipongeza TARURA kwa kuendelea kung’arisha mji wa Bukoba hasa mitaa ya pembezoni kwa kuwawekea lami na taa za barabarani jambo ambalo linakuza uchumi wao kwa kufanya biashara za usiku na mchana.

Meneja wa TARURA Wilaya ya Bukoba, Emmanuel Yohana amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa awamu tatu na lengo kuu ni kuendelea kuweka lami katika mitaa na kupendezesha mji wa Bukoba.

Amesema mradi huo umefika asilimia 40 na ulianza kutekelezwa Septemba mwaka 2024 na utakamilika Novemba 2025 ili wananchi wa kata kashai na Nshambya wanaunganishwa na Barabara hiyo waendelee kuitumia barabara kwa urahisi pamoja na wananchi kufanya biashara nyakati za usiku baada ya kuwekewa taka



