Wanawake wanavyochangamkia kilimo ikolojia kuzalisha mazao ya asili
KILIMO ikolojia ni mfumo wa ukuzaji mimea au mifugo kwa njia jumuishi inayowezesha kufikia ustawi wa kijamii kimahitaji, kimazingira na kiuchumi.
Hutafuta kuboresha mwingiliano kati ya mimea, wanyama, binadamu na mazingira. Kupitia mfumo wa kilimo ikolojia, jamii inajihakikishia usalama wa chakula na utunzaji wa mazingira. Mfumo huu licha ya kuhakikisha usafi na usalama wa vyakula, pia husaidia katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Hivyo, kupitia mfumo wa kilimo ikolojia, jamii inalenga kulinda na kuhifadhi mazingira na kuongeza ufanisi katika uzalishaji kwa kutumia rasilimali zinazomzunguka mkulima kwa gharama nafuu, hivyo kuboresha kipato na ustawi wa mkulima.
Katika kufanikisha kilimo ikolojia cha mazao ya asili, mtandao wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali wa Pelum Tanzania umetoa ufadhili wa Sh milioni 402.2 kwa mashirika ya kijamii yaliyopo katika Halmashauri za Wilaya ya Morogoro, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Gairo, Mvomero na Kilosa.

Ofisa Programu, Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wa Pelum Tanzania, Anna Marwa anasema fedha hizo zilitolewa kwa mashirika ya kijamii yasiyo ya kiserikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, ikiwamo ya kilimo ikolojia cha mazao ya asili.
Kwa mujibu wa Anna, ufadhili huo umetolewa katika kipindi cha mwaka 2024 kutekeleza miradi mbalimbali, ikiwamo ya kilimo cha ikilojia cha mazao ya asili. Miradi hiyo ni pamoja na ya utunzaji na usimamizi wa maliasili, utoaji wa elimu kuhusu mabadiliko ya tabianchi na uelimishaji juu ya kanuni na mbinu za kilimo ikolojia cha mazao ya asili.
Anasema Pelum Tanzania pia inatoa ruzuku kwa mashirika madogo kupitia utekelezaji wa mradi wake wa Imarika katika maeneo matatu. Maeneo hayo ni kilimo ikolojia cha mazao ya mbegu za asili, uwezeshaji wanawake na masuala ya mazingira.
Anasema Pelum Tanzania imekuwa ikihusika kuhamasisha matumizi ya mbegu za asili katika kilimo. Kwa Mkoa wa Morogoro, zimeundwa benki 12 za mbegu asili katika wilaya za Morogoro, Kilosa na Gairo. Anasema kuundwa kwa benki hizo za mbegu za mazao ya asili ni sehemu ya mkakati wa kutunza bayoanuai ya mbegu na kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa upatikanaji wake kwa urahisi.
Anna anasema katika kuhamasisha uwezeshaji wanawake kiuchumi kupitia kilimo cha ikilojia, vikundi vya wanawake na vijana vimeweka fedha takribani Sh milioni 53.5. Fedha hizo huwasaidia kwa kukopeshana na kuwekeza katika kilimo cha ikolojia.
“Tumeongeza uelewa wa matumizi ya mbegu za asili ambao hivi sasa umesaidia baadhi ya mbegu za asili kupata usajili na kuruhusu wakulima kuzizalisha,” anasema. Kwa mujibu wa Anna, kwa sheria za Tanzania, mbegu za asili ambazo hajafanyiwa usajili hazirihusiwi kuuzwa lakini kwa sababu zimesajiliwa, zikiwemo za mahindi, zitawezesha wakulima kuzalisha vizuri na kufanya mauzo.
Ofisa Kilimo wa Pelum Tanzania, Zakia Mohamedi anasema wanawake katika vijiji vinne vya Kata ya Tomondo, Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wanatekeleza Mradi wa Mwanamke wa Kijijini ili kuleta mabadiliko. Wanawake hao waliojiunga katika vikundi ni kutoka vijiji vya Lukonde, Kikundi, Kungwe na Vuleni wanaojishughulisha na kilimo ikolojia cha mazao ya asili.
Aidha, wamefundishwa namna ya kuongeza thamani ya mazao hayo. Zakia anasema huo ni mpango wa kuwezesha wanawake wa vijijini, kupitia mafunzo waliyopata kuhifadhi virutubishi ambavyo vingepotea endapo mazao ya asili yasigeongezwa thamani na kutunzwa.
Anasema wanaposisitizia wakulima kutumia kilimo ikolojia, ni muhimu kutambua kuwa kinawapa wakulima nafasi ya kuwa na uwezo wa kuchanganya mazao ya asili zaidi ya moja shambani kwake. “… kilimo hiki kinaelekeza namna wanavyoweza kupanda kwa eneo dogo na kuzalisha kwa wingi mazao tofauti, huku wakirutubisha udongo kwa matumizi ya baadae,” anasema.
Zakia anasema kilimo cha ikolojia cha mazao ya asili kimeiwezesha jamii ya Kata ya Tomondo kupata lishe bora kupitia kilimo hicho. “Wakulima wameweza kuongeza uzalishaji na kupata chakula cha kutosha ambacho wanakipeleka shuleni kuchangia watoto wapate mlo shuleni,” anasema.
Mkulima wa Kilimo Ikolojia katika Kijiji cha Lukonde, Kata ya Tomondo, Mwanahamisi Rajabu anasema baada ya kupata mafunzo ya kilimo ikolojia kupitia Pelum Tanzania chini ya Mradi wa Mwanamke wa Kijiji, wanawake kijijini hapo wameleta mabadiliko kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya asili.
Mwanahamisi ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Mbegu za Mazao ya Asili wa Kikundi cha Juhudi, ni kati ya wanamke wa kijijini hapo walionufaika na mradi huo. Anasema baada ya kupata mafunzo ya kilimo ikolojia kupitia Pelum Tanzania chini ya mradi huo, wanawake kijijini hapo wameleta mabadiliko kwa kuongeza uzalishaji mkubwa wa mazao ya asili.

Anasema wanawake wa kijiji hicho ni wazalishaji wa mbegu za asili za aina mbalimbali, zikiwemo za mtama, kunde, mbegu za maboga zinazoitwa ‘kikwangule’, mchicha aina ya ‘bwasi’ na nyingine ambazo walizorithi kutoka kwa wazee wao.
“Tunazo mbegu za asili, ikiwemo ya ‘majibwa’ ambao ni mtama mzuri, kwa sababu wakati wa kupikwa hata ukiwa na maji madogo huwahi kuiva jikoni, ndiyo maana ya kuitwa majibwa,” anasema Mwanahamisi. Anataja mbegu nyingine ya asili ya kunde aina ya ‘kikong’oro’, akisema ni mbegu isiyochakaa haraka shambani na inazaa kwa wingi.
Nyingine ni mbegu ya mbaazi inayojulikana kwa jina la ‘kucha la simba’ anayosema inazaa vizuri, huvumilia ukame na imara zaidi, ndio maana wazee wao wakaiita jina hilo. Mwanahamisi anataja mbegu ya asili ya mchicha inayoitwa bwasi ambayo hujiotea wakati wa mvua na katika maeneo yenye unyevu.
“Mchicha huu unapendwa na wananchi, kwani ni mtamu ukiula baada ya kupikwa, tofauti na mchicha mwingine na unasaidia sana kwa afya za watu,” anasema. Mwanahamisi anasema baada ya kupata elimu kutoka kwa watalamu wa uzalishaji mazao ya asili, kumekuwa na mwamko wa wananchi kuzalisha mazao yanayotokana na mbegu za asili.
Anashauri wanawake wanaoishi vijijini pamoja na vijana kutobweteka kusubiri ajira, kwa kuwa ajira wanazo katika maeneo yao. Anashauri wajikite katika uzalishaji wa mboga zinazotokana na mbegu za asili, akisema zinapatikana kirahisi na mazao yatokanayo na mbegu hizo yana bei nzuri na masoko ya uhakika.
Mwanahamisi anasema kutokana na uendelezaji wa kilimo ikolojia, kwa sasa wanakijiji wa Kata ya Tomondo wameongeza ari, kutunza mazingira na vyanzo vya maji.
“Tumeunda kamati za mazingira zinazosimamia jambo hili na hata wakulima wa mboga nyakati za ukame, tunatumia maji ya visima vilivyochimbwa kutokana kukosekana kwa mto, kuendeleza uzalishaji wa mazao haya,” anasema.




I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
.
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com