Wanu asisitiza ujuzi kwa vijana

NAIBU Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafi dh Ameir amesisitiza kuwa Tanza nia itaendelea kuwa taifa lenye vijana wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ili kutatua changamoto ya ajira ikiwamo ukuzaji wa uchumi.

Pia, ameiagiza Taa sisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) kuendelea kufanya bunifu na tafiti unaoendana na mahitaji ya jamii ili kutatua changamoto zilizopo na kujibu ajira kupitia tafiti.

Wanu alisema hayo jana wakati alipotembelea NM-AIST kujionea bunifu mbalimbali na ujenzi wa hos teli ya wanafunzi ili kuweze sha wanafunzi wanaosoma katika taasisi hiyo kupata eneo la kuishi.

Alisema serikali imeweka kipaumbele kusimamia mageuzi ya teknolojia zinazoi buka ikiwamo kujenga uwezo wa nchi katika teknolojia ya akili unde, sayansi shirikishi inayoandaa wataalamu kupitia Ufadhili wa Masomo wa Samia kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Tume ya Sayansi na Teknolojia (CoSTECH).

“Taifa linawategemea watafiti na wabunifu katika mageuzi ya kidijiti, pia nyie wanafunzi mliopata ufad hili huu zingatieni maadili ya watanzania ikiwemo mila na desturi zenu, hakikisheni taifa linawategemea, msiwe watumwa kwani programu hii inafungua njia nyingi za udahili na masomo duniani,” alisema Wanu.

Aliagiza wanafunzi 50 ku saidiwa na Taasisi ya Nelson Mandela kuomba ufadhili katika vyuo vikuu bora duni ani kwani serikali itaendelea kuhakikisha taasisi hiyo inaendelea kupewa mbinu zaidi katika mafunzo na bunifu za akili unde

Alitaka kasi ya mradi wa hosteli iongezwe ili ujenzi ukamilike huku changamoto ya fedha iliyobaki ikitatuliwa ikiwamo utafutaji wa vyanzo mbadala wa fedha kwa wa fadhili katika kuhakikisha miundombinu inaboreshwa.

Naye Makamu Mkuu wa taasisi, Profesa Maulilio Kipanyula aliwapongeza wanafunzi hao 50 kupitia kambi maalumu ya Ufadhili wa Masomo wa Samia katika Programu juu ya Sayansi ya Data, Akili Unde (IA) na Sayansi Shirikishi kwa kush irikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na CoSTECH.

Profesa Kipanyula alisema dhamira ya serikali kupitia NM-AIST ni kuendelea kuwaandaa vijana kuchochea mageuzi ya teknolojia nchini kwani kwa hivi sasa vijana hao wamepata ufadhili wa masomo Liberia, Afrika Kusini na Urusi ambako wanajiandaa kupata vibali vya kusafiri kwenda kusoma kozi hizo ili Tanzania iwe na wataalamu wengi zaidi.

Alisema vijana 10 kati yao wamepata ufadhili nchini Afrika Kusini. “Ninashukuru serikali kwa kutuamini na kutuwezesha, vifaa hivi ambavyo tutavitu mia vema katika masomo yetu na kutusaidia kusoma zaidi ili kugundua zaidi mambo yanayowezesha kutatua changamoto katika masuala mbalimbali,” alisema.

Programu hiyo ilianza Sep temba 15, mwaka jana ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa serikali wa kujenga wataal amu katika maeneo ya Sayansi ya Data, Sayansi Shirikishi na Akili Unde

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button