Wapewa mbinu kuepuka udumavu

LONGIDO: WANANCHI wanaoshi maeneo ya Pemberton wameagizwa kutumia makundi saba ya vyakula ili kuhakikisha wanaondokana na tatizo la udumavu.
Agizo hilo limetolewa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge, IsmailAlli Usi wakati wa maonesho ya masuala ya lishe ikiwemo kuzindua nyumba mbili za watumishi wa afya kata ya Kimokouwa wilayani Longido.
Ussi amesema ulaji wa vyakula sahihi utawezesha wananchi wanaoshi pembezoni kuondokana na udumavu kwa watoto ikiwemo kutumia tunda la britruti ili kuongeza damu pamoja na maofisa lishe wilaya ya Longido kuendelea kuhamasisha matumizi ya ulaji wa vyakula mbalimbali.
Awali akizundua nyumba mbili za watumishi wa afya kata ya Kimokouwa alisema serikali imejenga zahanati na vituo vya afya karibu na wananchi ili kuhakikisha wanapata huduma bora za afya
“Tuendelee kuwapa ushirikiano watoa huduma za afya lakini tuepuke malumbano yasiyo na tija ili kuhakikisha watoa huduma za afya wanatoa huduma bora za afya lakini maofisa lishe toeni elimu kwa wananchi ili wajue music kula vyakula vilivyopo katika makundi sita”
Aliipongeza halmashauri ya Longido chini ya Ofisa Lishe, Adelina Kahija kuendelea kutoa elimu sahihi ya lishe kwani kunabaadhi ya wananchi haswa maeneo ya vijijini bado hawatumii makundi sita ya lishe bora hali inayoleta changamoto za ukuaji haswa kwa watoto na damu kuwa ndogo na kusisitiza kauli mbiu ya “Mtaji ni Afya Yako, Zingatia unachokula,” izingatiwe katika ulaji bora wa vyakula.