Wapiga kura 175, 068 kupiga kura Ngorongoro

ARUSHA: MSIMAMIZI wa uchaguzi katika Jimbo la Ngorongoro mkoani Arusha, Emmanuel Mchome amesema katika jimbo hilo waliojiandikisha kupiga kura ni 175,068
Mchome amesema kuwa wapiga kura hao watapiga kura katika vituo 550 vilivyotengwa kwa ajili ya kupiga kura na vituo hivyo vitafunguliwa kuanzia saa 1 asubuhi na vitafungwa majira ya saa 10 jioni.
Alisema kutokana na jiografia ya jimbo hilo lenye kata 22 vifaa vyote vya uchaguzi vimeanza kusambazwa toka jana na leo ili kukabiliana na usumbufu usiokuwa wa lazima.
Mchome alisema nafasi ya wagombea udiwani matokeo yake yatatangazwa na msimamizi wa kata siku hiyo ya upigaji kura na matokeo hayo yatabandikwa katika ubao wa matangazo wa kituo husika cha kupiga kura.
Alisema nafasi ya ubunge itatangazwa katika Jimbo baada ya kukusanywa matokeo katika kata zote 22 na matokeo hayo yatatangazwa na yeye kama msimamizi wa uchaguzi na sio mtu mwingine.
Katika jimbo la Longido wapiga kura waliojiandikisha kupiga kura kesho ni wapiga 106,512 na watapiga kura katika vituo 314 na vifaa vimeanza kusambazwa katika vituo kuanzia jana na kwa kufanya hivyo ni kutokana na joografia ya miundombinu ya jimbo hilo.
Hayo yalisemwa na Ofisa Uchaguzi wa Jimbo la Longido, Erick Tinkaligaile na kusema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kujichobaki ni upigaji kura na vituo virafunguliwa majira ya saa 1 asubuhi na kufungwa saa 10 jioni.
Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Arumeru Magharibi,Stedvant Kileo amesema kuwa katika jimbo hilo kuna jumla ya vituo vya kupigia kura 717 na wapiga kura 279,252.
Kileo alisema jimbo hilo lenye kata 27 tayari vifaa vyake vimeshasambazwa kwenye vituo vyote 717 vya jimbo hilo na kwa kufanya ni kutaka vifaa hivyo kufika kwa wakati kabla ya upigaji kura kuanza kesho majira ya saa 1 asubuhi na kufungwa saa 10 jioni.
Katika Jimbo la Monduli lina wapiga kura 140,113 ambao wanatarajia kupiga kura katika vituo 400 vya jimbo hilo na vifaa tayari vimeshasambazwa na wasimamizi wasaidizi wa jimbo hilo.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern……………………………………. http://Www.Cash43.Com
Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
.
More Details For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com