Wasira akemea makundi CCM

ARUSHA; MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira ameagiza wanachama wa chama hicho wavunje makundi ya wakati wa mchakato wa kupata wagombea ubunge na udiwani.
Wasira alisema hayo wakati wa mkutano na wanachama cha chama hicho wakiwemo viongozi wa chama hicho jijini Arusha.
Wasira alihimiza wana CCM kutafuta kura na kuhamasisha wananchi kupiga kura ili kupata ushindi.
Alisisitiza wanachama kutogawanyika kwa sababu ya makundi yao badala yake waungane ili kuhakikisha CCM inaendelea kuongoza dola.
Wasira alisema Mkoa wa Arusha una wapigakura milioni 1.5 hivyo wanachama wa CCM wana wajibu wa kufanya kampeni ngazi ya kata na ubunge.
“Kama ulikuwa na mgombea wako hakuchaguliwa acha aliyechaguliwa afanye kazi, hiki chama kina watu wengi na hata ukiwaondoa utawakuta wengine wapo wazuri sana hivyo tuwaunge mkono walioshinda,” alisema.
Wasira alisema CCM ina historia na kuleta ukombozi hivyo si sawa mtu kujitokeza kukisema chama kuliko wanachama wenyewe.
“Hivi huyo anayekisemea chama anapata wapi ujasiri ilhali wenye chama wapo na wanajua historia yake kwani CCM inashika dola sababu ina kazi ya kufanya ikiwemo kusimamia ustawi wa watu, tuungane tusigawanyike ili tushinde kwa kishindo Oktoba mwaka huu,” alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla alisema ni muhimu vyama vyote vya upinzani vikashiriki kuhakikisha demokrasia inakua zaidi ikiwemo kulinda amani.
Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Musa Matoroka alisema hali ya kisiasa kuelekea katika uchaguzi ni shwari.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com