Wasira amsifu Samia utafsiri Ilani ya CCM

MOSHI : MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira amesema kwa miaka minne na nusu, Rais Samia Suluhu Hassan ametafsiri maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM kuleta maendeleo na kutatua changamoto za wananchi.

Alisema kutokana na kazi nzuri aliyoifanya na kwa kuwa Ilani mpya ya Uchaguzi ya CCM 2025-2030 Watanzania wana kila sababu ya kumpa nafasi kwa kuwa ana uzoefu wa kuongoza na kuipeleka mbele zaidi Tanzania. SOMA: Samia: Ilani ya CCM imezingatia maudhui Dira ya maendeleo 2050

Wasira alisema hayo jana mjini Moshi alipokuwa akizungumza na wana CCM kutoka Jimbo la Vunjo na Moshi Vijijini akiwa katika ziara ya kumnadi na kumwombea kura mgombea urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan. “Mama Samia kwa niaba ya chama chetu ametekeleza wajibu wa kusaidia kuleta maendeleo. Sasa tunakwenda katika uchaguzi, hili ni ombi mahususi ambalo nalileta kwenu wananchi wa Moshi na Kilimanjaro yote mkumbukeni na mpeni kura za kishindo Samia Suluhu Hassan.

“Amefanya kazi kubwa na ilani hii mpya nayo ina mambo makubwa yanahitaji mtu mwenye uzoefu kusimamia na kusukuma maendeleo ya nchi yetu kutoka yalipo kwenda mahali mbele. “Wewe una gari jipya unatafuta dereva unachukua mtu hana leseni ataiangusha! Hana leseni unampa Scania aendeshe unasema huyu mimi ni ndugu yangu, jirani, wacha ujirani uendelee lakini kama si dereva gari mkabidhi mwenye leseni. Samia ana leseni tena si ndogo, kubwa,” alisema Wasira.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button