Wataalam 34 ununuzi ugavi wawajibishwa

BODI ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imewawajibisha kinidhamu wataalam 34 wa maeneo mbalimbali nchini ambao walibainika kufanya kazi kwa uzembe bila kuzingatia taaluma na kuisababishia hasara Serikali na watu kukosa huduma iliyokusudiwa kutolewa kwao.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo ,Godfred Mbanyi  amesema hayo Januari 9, 2025  mjini Morogoro kwenye Kikao cha wajumbe wa Bazara la wafanyakazi la Bodi hiyo kwa ajili ya kujadili na kupitia wasilisho la Menejimenti kuhusu makadirio ya Bajeti ya mwaka wa Fedha 2025/2026/

Mbanyi amesema bodi hiyo imekuwa ikichukua katua kali kwa wataalam wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ambapo hadi kufikia Desemba mwaka jana (2024) wataalam 34 waliokuwa maeneo mbalimbali nchini wamechukuliwa  hatua za kinidhamu.

Advertisement

“ Kwa njia moja ama ninyine wataalam hawa walichangia miradi kutokamilika kwa wakati, kukamilika chini ya kiwango na kutokamilika kabisa na hatimaye kupoteza fedha za serikali na pia kusababisha hasara na watu kukosa huduma ambapo lengo kuu Serikaki ni kutoa huduma kwa watu,” amesisitiza Mbanyi.

Mbanyi amesema kutokana na hatua mbalimbali zinazochukuliwa, odi kwa sasa inajuvunia watalamu wake kuanza kuelewa ya kwamba serikali na nchi inawatengeea kwenye michakato ya manunuzi yenye kufuata sheria, utaratibu na maadili.

Amesema kuwa kupungua huko kunatokana na Bodi kujikita katika masuala ya kusimamia maadili ya wataalamu wake  na kuchukua hatua dhidi ya wale wanaokwenda kinyume na taaluma zao

“ Siku za nyuma bodi ilikuwa ikipata changamoto nyingi , lakini kwa sasa hata kesi mbalimbali  kutoka kwa viongozi wetu wakuu walizokuwa wakiziibua wakiwa wanafanya ziara mbalimbali zimepungua” amesema Mbanyi.

Amesema kuwa kila mwaka bodi inachukua hatua kwa wataalam wanaokiuka utaratibu na kwa sasa wamenza kuogopa na kufanya kazi kwa uaminifu.

Mbanyi amesema wengi wanafanya vitu si kwamba walitaka kuiba bali kulikuwa na uzembe wa makusudi katika kutekeleza sheria na matokeo yake tunaopata hasara ni Watanzania .

“ Kama mradi uliokuwa unajengwa ni daraja, shule ama kituo cha afya ni mali ya watanzania  na mtaalam anapofanya uzembe ,sisi Bodi unatushughulika naye, hatuangalii mtu ( Mtaalam) kala rushwa ,tunaangalia kwamba hukutelekeza wajibu wake kwa utaratibu na miongozo ya taaluma tunashughulika na huyo mtaalam,” amesema .