Simiyu yapewa mafunzo ya uhifadhi

SIMIYU : BAADHI ya wajumbe wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii wamewasili mkoani Simiyu kwa ajili ya kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii.

Elimu hiyo inalenga kuwawezesha wananchi kujikinga na wanyama wakali na waharibifu,Taratibu na kanuni za kumiliki Nyara za Serikali pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya jamii na mamlaka za hifadhi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bi. Prisca Kayombo, amepokea rasmi timu hiyo ya wataalam leo tarehe 04 Oktoba,2025 tayari kuanza utekelezaji wa majukumu yao mkoani humo. SOMA: Maliasili yapongezwa kutekeleza maono ya Rais Samia

Timu hiyo ya elimu kwa jamii inaundwa na wataalam kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Idara ya Wanyamapori, Mamlaka ya Usiamizi wa yaWanmapori – TWA Apamoja na maafisa Wanyamapori kutoka halmashauri husika.

Zoezi la utoaji elimu hiyo litafanyika katika maeneo yenye changamoto kubwa za wanyama wakali, hususan fisi waliouawa hivi karibuni katika Wilaya za Busega na Itilima.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button