Wataalamu wa ganzi, usingizi kujifunza njia za kisasa MOI

DAR ES SALAAM: TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kwa kushirikiana na wataalamu kutoka India leo wameanza kutoa mafunzo ya kutumia njia za kisasa kwa wataalamu 80 wa dawa za usingizi tiba pamoja na ganzi ili kupunguza gharama na muda wa wagonjwa kukaa hospitali.

Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Ganzi na Usingizi Salama, Naima Zakaria amesema kwa njia za zamani wanazotumia ya dawa ya usingizi za kulaza moja kwa moja gharama ni Sh 100,000 wakati kwa njia ya kisasa ya dawa za kuziba mishipa haizidi Sh 20,000.

“Changamoto kubwa zaidi ni matumizi ya njia ya kisasa kwani sasa tunatoa dawa ya usingizi kwa njia mbili na huko duniani wameendelee wako njia hadi za tano na

Amesema mafunzo hayo ya kisasa yatarahisisha utoaji wa huduma ambapo sasa wagonjwa watakaa hosptali muda mfupi na gharama kupungua.

“Ukimlaza moja kwa moja anachukua muda kukaa hospitali zaidi hata ya siku mbili wangempa ganzi ya mkono peke yake hata siku ya pili anaondoka ,”amefafanua.

Akizungumza wakati wakufungua mafunzo hayo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya, Dk Ahmad Nyembea amesema lengo ni uboreshaji wa huduma za upasuaji ambazo zimeongezeka hadi vituo vya afya na huduma hizo zinahitaji wataalamu.

Amesema wataalamu hao watajifunza kwa vitendo ili kujengewa uwezo zaidi ambapo mafunzo kama hayo yatatokea mara kwa mara huku wataalamu wata India watakuja huku n awa Tanzania wakienda India.

“Lengo ni kupata wataalamu bora zaidi na mtu akifanyiwa upasuaji uwe wa hali ya juu ,Kutokana na vituo kuongezeka wataalamu wanahitajika zaidi na vyuo vimeongezeka tunategemea mwaka 2028 tuwe na wataalaamu 300 kutoka 80,”amesisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MOI,Dk Mpoki Ulisubisya amesema huo ni utaratibu uliobuniwa na kutekelezwa na Chama cha wataalamu wanaotoa dawa za usingizi tiba pamoja na gazi kwa kushirikiana na wataalamu mahiri kutoka India ambao wamebobea katika fani hiyo.

“Watawafundisha wataalamu namna ya kutoa dawa kutumia mbinu za kisasa zaidi kuliko zile ambazo tumezoea kuzifanya katika nchi ,tunajifunza mbinu za kisasa zaidi mfano mgonjwa akija anahitaji matibabu ya mkono tutaweka gazi ya mkono na sio mwili wote.

Ameongeza “Au anamaumivu ya muda mrefu hata kama akipewa dawa za kuzuia maumivu hazimsaidii tunataka tujifunze namna ya kutoa huduma kwa watu hao au kama tunataka kuchoma sindano za ganzi lakini mishipa hatujui iliko katika mwili tutumie mawimbi ya sauti tuweza kupata na kupeleka dawa.

Dk Ulisubisya amesema kuna namna ya kutoa dawa ya usingizi ambayo inakuwa na lengo maalum katika ubungo ambayo inapeleka dawa inayohitaka watajifunza katika mafunzo hayo.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho wa vyama vya Madaktari Bingwa wa Usingizi Duniani(WFSA) Dk Balavenkata Subramanian amebainisha kuwa wamekuja kushirikana na kujifunza kutoka kwa wataalamu wa ndani na wan je kwani nchi zao zinakabiliana na changamoto zinazofanana kama nchi zinazoendelea kama vile uhitaji wa madawa na miundombinu ambayo sio mingi sana.

“Na katika hilo tunataka wagonjwa wakae vizuri baada ya upasuaji na wanapata huduma bora kwasiku tatu tunafurahi tutakuwa tunashirikiana katika kubadilishana ujuzi na maarifa wa teknolojia mpya kwa kutumia vifaa.

Amesema wataalamu watajifunza teknolojia mpya itakayofanya huduma kuwa salama zaidi.

“Nawapongeza chama cha hapa Tanzania huu ni mwanzo wa safari ya Tanzania na India kujifunza Pamoja na kushirikiana,”amesisitiza.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button