Watakiwa kuongeza uelewa usawa wa kijinsia

KILIMANJARO; JAMII imetakiwa kuongeza uelewa kuhusu haki za binadamu na usawa wa kijinsia, ili kulinda na kutetea haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Elimu wa Shirika la Tusonge, Consolata Kinabo, wakati wa semina ya kukuza usawa kwa kutumia haki za binadamu kwa makundi ya wanawake, watu wenye ulemavu na watoto katika Kata ya Bomambuzi, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.

Kinabo amesema kwa mujibu wa tafiti waliyoifanya mwaka 2019, wanawake wengi bado wanaathirika na ukatili wa kijinsia na kingono jambo linalosababisha washindwe kushiriki katika shughuli za kijamii kukuza maendeleo yao na kujithamini.

Aidha wamebaini kuna wanaume ambao wanaathirika na ukatili, hivyo wanahakikisha jamii yote inakuwa salama dhidi ya vitendo hivyo kwa kuwa haki za binadamu ni kwa watu wote.

“ingawa walengwa wa mradi ni watoto na wanawake pia tumewafikia wanaume kwa sababu wote wakiwa na uelewa familia inakuwa salama lakini ukimuelimisha mmoja  inakuwa haina tija,” amesema

Baadhi ya wanawake kutoka Kata ya Bomambuzi, wamewataka wanawake waondoe hofu, wajiamini, washiriki kwenye vikao mbalimbali vikiwemo vya serikali za mitaa na kata na kutoa maoni.

Kwa upande wa wanafunzi walioshiriki kwenye semina hiyo, wameomba watoto wapewe haki ya kutoa maoni katika familia na vikao vya kijamii.

Mradi huo umewafikia watu zaidi ya 1300 katika mkoa wa Kilimanjaro na Arusha, wakiwemo viongozi, wanawake na watoto na unatarajia kuisha mwaka 2024.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button