Watanzania kula maisha Dubai ‘Valentine Day’

WATANZANIA Kadhaa watapata nafasi ya kusherehekea siku ya wapendanao ‘Valentine Day’ wakiwa nchini Dubai.
Hatua hiyo ni baaada ya Kampuni ya Simu ya Halotel kuwakabidhi tiketi za ndege kwa washindi wa ‘Vuna Pointi Twenzetu Dubai.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 13,2025 makao makuu ya kampuni hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Roxana Kadio amesema kampuni hiyo inajivunia kutangaza kumalizika kwa kampeni hiyo ya kipekee inayowakutanisha watanzania hao nchini humo.

“Kampeni ya Vuna Pointi Twenzetu Dubai ni kampeni ambayo ilikua inamuwezesha mteja kuvuna pointi kupitia namba ya bahati na kupata nafasi ya kujishindia nafasi ya kwenda Dubai na Mwenza wake au mtu yeyote atakayemchagua,”amesema Kadio.
Ameongeza,”kufikia tamati imeweza kuwapa ushindi kwa wateja wawili wa Halotel ambao wamepata bahati ya kwenda Dubai kwa siku tatu msimu huu wa wapendanao,”
Amesema kampeni hiyo ni sehemu ya dhamira kwa Kampuni hiyo kuimarisha uzoefu wa wateja na kuwalipa wateja wao waaminifu wananachofanya kupitia shindano hilo ni kuwapa nafasi ya kuishi na kupata uzoefu wa Dubai, mji maarufu kwa anasa, tamaduni, na uvumbuzi.

Mwakilishi kutoka Kitengo cha Huduma kwa Wateja Halotel,Sharon Kessy amesema kampuni hiyo inaendelea kuimarisha sifa yake kama chapa inayojali wateja kwa kutoa sio tu huduma bora za mawasiliano bali pia uzoefu unaoboresha maisha ya watumiaji wake hivyo
Jamii ijiandae kushiriki mashindano mengine ya kuvutia mwaka huu.
Naye Mshindi wa tiketi hiyo Raphael Myombo amesema ndoto yake imetimia kwani hakuwahi fikiria kama angeweza kufika Dubai lakini kupitia Halotel amefanikiwa.



