Watanzania washauriwa kuiamini CCM

TANGA: Watanzania wameshauri kuendelea kukiamini Chama cha Mapinduzi (CCM) kutokana na dhamira yake ya kuendeleza kulinda na kiutunza Amani ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti CCM Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahaman wakati wa uzinduzi wa kampeni ngazi ya Mkoa wa Tanga iliyofanyika wilayani Mkinga.

Amesema kuwa Rais samia amekuwa akifanya juhudi kubwa ya kuhakikisha anailinda amani ya nchi hii kama ambavyo alivyorithi kutoka kwa watangulizi wake.

“CCM tunapowaomba muendelee kuchagua chama hiki ni kutokana na namna bora ambayo tunatumia katika kuhakikisha amani ya nchi inadumishwa ndani ya nchi hii, “amesema mwenyekiti huyo.

Amesema kuwa busara,hekima na uvumilivu wake ambao umeonyeshwa na Rais Samia ni kielelezo tosha cha wananchi kuendelea kumuamini na kumrudisha tena Ikulu ili aweze kuendelea kudumisha amani ya nchi hii.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Mkoa wa Tanga, Omar Ayoub amesema kuwa wananchi wanakila sababu za kuwaunga mkono wagombea wa chama hicho kwani ndio chama ambacho kimeweza  kutoa wagombea kwa kufuata  miongozo sahihi ndani ya nchi hii.

Pia Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Tanga, Ramadhani Omar amesema kuwa Rais samia ameiletea sifa nchi kutokana na mahusiano mazuri ambayo ameyajenga na  nchi za nje.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button