Watia nia CCM waonywa dhidi ya rushwa

TANGA: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga na Mjumbe wa Kamati Kuu Taifa, Rajabu Abraham amesema chama hicho hakitasita kuwachukulia hatua za kisheria watia nia za uongozi watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati wa ziara ya kukagua ukarabati wa ujenzi unaondelea wa ofisi ya chama hicho ngazi ya mkoa. Amesema kuwa fedha sio kigezo cha mgombea kuchaguliwa katika nafasi ya uongozi hususani ya kuwatumia wananchi.

“Kama wewe na fedha zao umekuja kwania kutaka uongozi kwa kutumia rushwa tukikubaini utakuwa umekosa sifa lakini na hatua kali za kisheria zitaweza kuchukuliwa juu yako,”amesema mwenyekiti huyo.

Akizungumzia ujenzi wa ofisi ya chama, amesema kuwa ni sehemu ya mikakati ya chama hicho ya kuhakikisha watumishi wao wanafanyakazi katika mazingira rafiki ya kuwahudumia wananchi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Mwenyekiti wa Chama Taifa ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan.

SOMA ZAIDI

Takukuru Iringa yawahoji watia nia CCM

“Tunakwenda kujenga ofisi na nyumba za watumishi wetu Ili waweze kufanana na hadhi ya chama hiki kwani kina historia kubwa ya uongozi hivyo ni muhimu tuweke mazingira mazuri ya kazi Kwa watendaji wetu”amesema.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo meneja mradi mhandisi Amon kyomo amesema kuwa mradi huo umeweza kufikia asilimia 97.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button