Watoto wenye vichwa vikubwa ,mgongo wazi kutibiwa bure MOI

TAASISI ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) Oktoba 25 inatarajia kufanya kambi maalum ya matibabu bure  kwaajili ya watoto waliozaliwa wakiwa na tatizo la Mgongo wazi na Kichwa kikubwa nchi nzima.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara ya Watoto na Daktari Bingwa wa Mifupa,Ubongo na Mishipa ya Fahamu,Dk Hamis Shaban amesema kambi hiyo inafanyika ikiwa ni maadhimisho ya siku ya watoto  wenye tatizo hilo.

Amesema kambi hiyo maalum  inadhaminiwa na Taasisi ya Mo Dewji Foundation na wadau wengine. “Tutawafanyia uchunguzi na matibabu bure hivyo tunawaalika wazaziza walete watoto wao siku ni tarehe 25 hapa MOI kuanzia asubuhi tutaona watoto wote nchi nzima,”amesisitiza Dk Hamisi.

DK Hamisi amebainisha kuwa katika kila vizazi 1,000 watoto watatu wanzaliwa na tatizo hilo huku kwa kila mwaka ni watoto 4,800 na MOI kwa wiki mmoja wanaona watoto 140. “Sababu kuu ni utapiamlo kwa akinamama kabla ya kupata ujauzito,utapiamlo huu ni ukosefu wa madini ya folic acid kinamama hawali vyakula vinavyotakiwa.

Ameongeza “Tunawashauri akinamama kabla hawajabeba mimba wahudhurie kliniki  wapate ushauri kwa wataalmu afya,kuna vyakula kama mbogamboga,matunda,vyakula vyenye nyuzi nyuzi,maziwa na pia kuna vidonge. Amesema hivi sasa kuna Unga wa ugali ambao umeongezwa virutubisho hivyo ni muhimu kinamama kuupata kwani yanamadini muhimu kuzuia tatizo hilo. “Watoto waletwe wanatibiwa na ulemavu unaisha kabisa tusifiche watoto hao wala tusiwanyanyapae huduma tunatoa bure hapa MOI,”amesisitiza.

Aidha amewashukuru wadau wanaoshiriki kufadhili kambi hiyo bure wakiwemo Mo Dewji Foundation  na wadau wengine wa ndani na nje ya nchi. SOMA: Watoto sita wenye vichwa vikubwa kulipiwa matibabu

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button