Watu milioni 5 hufariki tezi dume kwa mwaka EAC

DAR ES SALAAM: ZAIDI ya wanaume milioni tano hufariki kila mwaka katika ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na saratani ya tezi dume, huku sababu kubwa ikiwa ni mabadiliko ya umri.

Takwimu hizo zimetolewa leo Oktoba 15,2025 na Mkurugenzi wa Hospitali ya Heameda, iliyopo Bunju, Wilaya ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam, Dk Hery Mwandolela wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya miaka 15 ya utoaji wa huduma katika hospitali hiyo yatakayofanyika Oktoba 20 mwaka huu.

“Tezi dume ni tatizo linaloongezeka kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya umri. Katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki, changamoto hii inaongoza kuwa na wagonjwa wengi, huku ongezeko la ukubwa wa tezi yenyewe na saratani likiathiri zaidi na kusababisha vifo hivyo,” alisema Dk Mwandolela.

Aliongeza, “Takribani wagonjwa milioni 10 kila mwaka duniani kote hufariki na kati ya hizo nusu ni saratani ya tezi dume. Hata hivyo, nchini Tanzania takwimu hazijapatikana kikamilifu. Hivyo, suala hili linahitaji kufanyiwa kazi kwa kutoa ushauri wa kufanya vipimo mapema ili kuokoa maisha na nguvu kazi ya taifa.”

Akizungumzia magonjwa ya moyo, Dk Mwandolela ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya moyo alisema kuwa kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya mwaka 2025, wagonjwa milioni 20 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa ya moyo, sawa na asilimia 60 ya vifo vinavyotokea.

Amesema Hospitali hiyo imeandaa kambi maalumu ya madaktari kutoka India itakayofanyika kwa siku mbili ili kutoa huduma katika maeneo matatu makuu ambayo ni magonjwa ya moyo, mfumo wa fahamu, na magonjwa ya mfumo wa uzazi kwa wanaume, hasa yanayohusiana na ‘urology’.

“Tunatoa fursa kwa wananchi kupata huduma za kiafya za ubora mkubwa, tukichanganya wataalamu wa ndani na wageni kutoka nje ya nchi. Hii inahakikisha wagonjwa wanapata matibabu bora bila usumbufu wa usafiri au gharama kubwa. Huduma hizi zinajumuisha ushauri, vipimo, na matibabu ya moja kwa moja. Uwepo wa wataalamu hawa wa kimataifa unalenga kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu ya kisasa na ya kuaminika bila kulazimika kusafiri umbali mrefu kwenda India,” alisema Dk Mwandolela.

Ameongeza, “Tumelenga kwenye maeneo haya matatu makuu kwa sababu yanaathiri idadi kubwa ya wananchi. Magonjwa ya moyo yanasababisha vifo vya mamilioni kila mwaka duniani, na magonjwa ya mfumo wa fahamu na ‘urology’yanasababisha changamoto nyingi kwa watu binafsi na familia zao. Kwa kushirikiana na madaktari hawa tutaokoa nguvu kazi ya Taifa,”

Naye mmoja wa wagonjwa wanaopata huduma hospitalini hapo, Emmanuel Pula amesema kwa mara ya kwanza amepata matibabu ya kisasa karibu na nyumbani bila kulazimika kusafiri umbali mrefu.

“Madaktari wanaelewa mahitaji ya wagonjwa na wanaleta matokeo chanya. Nina matumaini makubwa, na ninaona afya yangu inaimarika kila siku naomba serikali iendeelee kuhamasisha watu kupata bima ya afya kwasababu kupitia bima unawezakupata huduma sehemu yeyote serikalini au binafsi kwa gharama nafuu,”amesema

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I get paid over (90$ to 500$ / hour ) working from home with 2 kids at home. I never thought I would be able to do it but my best friend earns over $22000 a month doing this and she convinced me to try. it was all true and has totally changed my life… This is what I do, check it out by Visiting Following web….
    .
    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button