Watuhumiwa 93 wa vurugu za uchaguzi wafikishwa mahakamani Mwanza

KESI inayowakabili watuhumiwa 93 kati ya 172 wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya uhalifu yaliyotokea wakati wa uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imeahirishwa hadi Desemba 2 baada ya upande wa mashitaka kudai kuwa upelelezi bado haujakamilika.
Watuhumiwa hao upande wa Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza wamekuwa wakifikishwa mahakamani kwa awamu, wakikabiliwa na mashitaka mbalimbali ikiwemo uharibifu wa mali na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Shauri hilo limetajwa leo Novemba 19, 2025 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Amani Sumari, ikiwa ni sehemu ya kesi zinazowakabili watu 172.
Upande wa mashtaka uliwakilishwa na Mawakili wa Serikali Bitunu Msangi na Prince Masawe, huku utetezi ukiwakilishwa na mawakili Duttu Chebwa na Beatus Linda kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS).




Arusha International Conference Centre Hospital
Chemba District Hospital
Muhimbili National Hospital
Saifee Hospital Tanzania
Rabininsia Memorial Hospital
Burhani Charitable Hospital
Haydom Lutheran Hospital