Watumishi watakiwa kufundwa sheria za kazi

ARUSHA: NAIBU Katibu Mkuu,Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Walemavu, Zuhura Yunus amewahimiza waajiri kote nchini kujenga utamaduni wa kuwajengea uwezo watumishi hususani mafunzo ya mara kwa mara na kuwakumbusha sheria na kanuni za kazi ili kuondoa migogoro katika maeneo kazi.
Zuhuru alisema hayo jana wakati akifungua semina ya waajiri serikalini na Viongozi wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania {TUGHE} alisema wajiri wote nchini wajenge utamaduni kwa watumishi wao katika kutoa mafunzo ya mara kwa mara lengo ni kuwajengea uwezo watumishi kujua wajibu wao kazini kwani kufanya hizo itakuwa ni mwarobaini wa kutibu na kuondoa migogoro.
Alisema watumishi pamoja na wajiri wakielewa vyema taratibu ,miongozo ,sheria na kanuni zinazosimamia utumishi wa umma na masuala ya ajira na mahusiano kazini haitakuwa rahisi kuzikiuka.
Naibu Katibu Mkuu huyo aliendelea kusema kuwa waliopata fursa ya mafunzo hayo watakaporejea maeneo ya kazi wahakikishe wanapata wasaa wa kuwajuza wengine yale aliyojifunza ili wote wapate kuwa na uelewa wa kutosha katika nmajukumu yao ya kazi.
“Serikali yetu inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan imekuwa mstari wa mbele kushughulikia na kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali za watumishi na kero zilizokuwa ni kikwazo zimepatiwaa utauzi”,aliongeza Yunus.
Katibu Mkuu wa TUGHE, Hery Mkunda alisema kuwa semina hiyo ya siku tano inashirikisha washiriki zaidi ya washiriki 800 alisema semina hiyo inalenga kujengeana uwezo,kubadilishana uzoefu na kujenga uhusiano chanya baina ya washiriki kukumbusha haki na wajibu wa mfanyakazi na maadili sehemu za kazi pia kuhamasisha ushirikishwaji.
“Mafunzo hayo yalianza mwaka 2018 ambapo jumla ya viongozi wa matawi na waajiri wapatao 4713 wamepata mafunzo kupitia semina hizo idadi ya washiriki imekuwa ikiongezeka kila mwaka na matunda yake yamesaidia kupunguza migogoro baina ya watumishi na waajiri,”alisema Mkunda.
Mkunda alisema TUGHE wanaipongeza serikali kwa namna ambavyo im ekuwa ikishughulikia changamoto mbalimbali za wafanyakazi na kusema wote ni mashahidi hoja nyingi zilizokuwa zikitukabili wafanyakazi zimepatiwa ufumbuzi na kuongeza ari na uwajibikaji wa wafanyakazi hapa nchini.
Mfano wa mambo machache moja ni ya hili la hivi karibuni ambalo ni nyongeza ya siku za likizo kwa wafanyakazi wanawake wanaojifungua watoto njiti sambamba na kuingiza mbadiliko haya kwenye sheria ya ajira na mahusiano kazini na suala hili lilianzia Baraza la wafanyakzi la TUGHE.